KANISA LA JEM GOSPEL MINISTRY LINALOFANYA HUDUMA ZAKE MKOANI MBEYA LIMESEMA CHANZO CHA UVUNJIFU WA AMANI WA MKOA WA MBEYA UNATOKANA NA BAADHI YA WATU WANAOJIFANYA NI VIONGOZI WA DINI KUJIHUSISHA NA VITENDO VIOVU NA KUTUMIA KIMVULI CHA KANISA KUJIFICHA.AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MBEYA JANA KIONGOZI WA KANISA HILO AMBAYE ALIJITAMBULISHA KUWA NI MTUME WA MUNGU ALISEMA KUWA WACHUNGAJI WASIOWEZA HUDUMA ZA KIROHO AMBAYO HUTUMIA MWAMVULI WA KANISA KUWATAPELI WAUMINI NI BORA WAKAINGIA KATIKA BIASHARA YA KUUZA MCHICHA NA KARANGA ILI KUJIONGEZEA KIPATO.ALISEMA KUWA MKOA WA MBEYA NI MIONGONI MWA MIKOA YENYE MAKANISA MENGI LAKINI HUDUMA ZA KIROHO KWA WAUMINI WALIOPO MKOANI HUMO HAIACHI ATHARI KUTOKANA NA KUENDELEA KUKITHIRI KWA MAUAJI YA USHIRIKINA NA VITENDO VIOVU.AIDHA MTUME HUYO ALIWATAKA WANAHABARI KUTOKATA TAMAA KUIHABARISHA JAMII KUTOKANA NA VITOSHO VINAVYOENDELEA DHIDI YAO KWAMBA UJUMBE UNAOTOKA KWA WANAHABARI NI UTUME KWA JAMII YA WATU WANYONGE. |
Post a Comment
Post a Comment