Ads (728x90)

MEYA WA JIJI LA MBEYA ATHANAS KAPUNGA:''Kuanzia sasa ushuru wa sh. 58,000 usitishwe, maana naona unatishia amani na utulivu wa jiji letu''

EMANUEL MBUZA: ''Nipeni nafasi ya kujieleza mbona hamnipi haki yangu''

MEYA WA JIJI: ''Hapana hapa sheria lazima ifuatwe tutafute utaratibu mzuri wa ukusanyaji ushuru usiwe kikwazo kwa wafanyabiashara''

MBUZA; ''Naomba na mimi niseme angalau kidogo!! kuhusiana na suala hili! mbona mnaninyima chance''


MBUZA ALIPATA NAFASI YA KUFUNGUKA MBELE YA WANAHABARI NA KUELEZA KUWA AMETUHUMIWA KWA MENGI LAKINI WENYE MATATIZO NI HALMASHAURI YA JIJI KUTOWEKA BAYANA SHERIA ZA UKUSANYAJI USHURU.

VIONGOZI WA CHAMA TAWALA NAO WALIKUWEMO NDANI YA NYUMBA KUWEKA BAYANA SERA NA ILANI ZA CHAMA KUHUSIANA NA UTOZAJI WA USHURU.

MAKAMU MENYEKITI WA WAMILIKI WA MAGARI GOLDEN MWAMAKULA;'' Tunaomba tuelezwe bayana suala hili maana linatukanganya, magari yetu yanatozwa ushuru kwa vitisho vijana wenye silaha wanasimama barabarani na kutulazimisha kutoa ushuru kwa nguvu kwanza ushuru wenyewe haulipiki tuna mizigo mikubwa ya ulipaji kodi katika jiji''

KAPUNGA: ''Hapa lazima tutumie busara maana hawa jamaa wamechachamaa vinginevyo itatuletea tabu hata kwenye vikao vya chama tawala''.

KAPUNGA; ''Jamani eeeh!! naomba mnisikilize! tumebaini lilipo tatizo, ushuru huu hauko kihalali, tutarejesha hili kwenye vikao,nasema hivi ushuru huo usitishwe mara moja, unaweza kusababisha kuvunjika kwa amani''





MBUZA; Sumatra ndio tatizo kubwa katika sekta ya usafirishaji.

''Hili lazima tuliweke sawa mie nalaumiwa bure wakati wenye makosa ni Jiji wenyewe.''


HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA IMESITISHA UTOZAJI WA USHURU WA SH.58,000 KWA MAGARI AINA YA CANTER NA FUSO KWA MADAI KUWA USHURU HUO UMEKUWA CHANZO CHA VURUGU NA UVUNJIFU WA AMANI KATIKA JIJI.AKIZUNGUMZA KATIKA UKUMBI WA MKAPA MEYA WA JIJI LA MBEYA ATHANAS KAPUNGA ALISEMA KUWA UTOZAJI WA MZABUNI ALIYEPEWA   DHAMANA YA KUKUSANYA USHURU HUO AMEKUWA AKILALAMIKIWA KUTUMIA UBABE HUKU VIJANA WANAOTUMIKA KUTOZA USHURU HUO WANADAIWA KUTUMIA SILAHA KWA KUJERUHI WAFANYABIASHARA. BW. KAPUNGA ALISEMA KUWA ILI KUEPUSHA MATATIZO HAYO KWA WANANCHI HALMASHAURI YA JIJI IMELZIMIKA KUSITISHA UTOZAJI USHURU NA KUREJESHA SUALA HILO KWENYE VIKAO VYA HALMASHAURI KULIANGALIA UPYA.KWA UPANDE WAO WAMILIKI NA MADEREVA WA MAGARI HAYO WALIDAI KUWA WATOZA USHURU WAMEKUWA WAKITEMBEA NA MAPANGA NA KUWALAZIMISHA WAFANYABIASHARA KUTOA USHURU AMBAPO MMOJA WAO ALIKATWA SIKIO AKISHINIKIZWA KULIPA USHURU HUO.KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI WA KAMPUNI INAYOTOZA USHURU HUO KWA MAGARI JIJI LA MBEYA EMANUEL MBUZA ALISEMA KUWA HALMASHAURI YA JIJI NDIYO ILIYOPASWA KUAINISHA NAMNA YA UTOAJI WA USHURU NA KUSEMA KUWA SHERIA ILIYOPO IMEJAA MAPUNGUFU YANAYOSABABISHA KUIBUKA KWA MGOGORO HUO BAINA YA WAFANYABIASHARA NA WATOZA USHURU.

Post a Comment

Post a Comment