WANACHAMA WA SIMBA WAMNG’OA RAGE WAMTUHUMU KUTOWAJIBIKA
Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Askari wakiangalia suala la usalama.
WANACHAMA wa klabu ya Simba, leo walifanya kikao cha dharura kwenye
Hoteli ya Star Light Mnazi Mmoja jijini Dar na kuung’oa uongozi wa
klabu hiyo uliopo madarakani chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage
kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao. Wanachama hao wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha kiongozi aliyejiuzulu hivi karibuni, Zacharia Hans Poppe. Wanachama hao wamesema wanatarajia kuitisha mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu inayoendelea ili kuepusha kuivuruga timu.(CHANZO GLOBAL PUBLISHERS) |
Post a Comment
Post a Comment