NI tukio lka
kusikitisha kwa kifo cha askari trafiki wa kike ambaye alikuwa akiongoza magari
eneo la Bamaga wakati msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukipita kwa mwendo kasi,
huyu hapa shuhuda wa tukio hilo anaelezea kama alivyoona;
‘’Ndugu
zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa
pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu
zikiwemo na ambulance.
Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili:
Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia
alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. Bila ya kuangalia nyuma ya
zile gari akaanza kuruhusu gari from Shekilango road na hapo ndipo Discovery 4
kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa
kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayo-cross from Shekilango.
Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya
kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic
huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni
kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi
niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio
nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona
maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.
Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama
nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta.(CHANZO GLOBAL PUBLISHERS)
|
Post a Comment
Post a Comment