| Kampuni
 ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, 
ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu
 juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo, (jana) imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya 
eneo la Jangwani.
 Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG  Zhang Chengwei David amesema 
upembuzi yakinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja 
mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na 
michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya 
Yanga.
 Zhang alisema kwamba 
kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali 
duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es 
salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya 
kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) 
uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 2010.
 Aidha
 Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium 
(jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi
 Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa 
kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba 
watazamaji 20,000.
 Katika 
uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa 
Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema 
wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi 
yakinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo 
ya ujenzi wa uwanja huo.
 Kufukwe alisema wamepewa nafasi 
ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na 
kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na 
mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba kwa ajili ya ujenzi wa
 uwanja mpya wa Kaunda.
 Akijibu swali
 la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za 
ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja mpya utajengwa na 
wanachama, wapenzi na washabiki wa klabu ya Yanga.
 Kwa
 mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa 
uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia 
utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 
kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.
 Kaunda
 stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye
 viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu 
maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari,
 eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja 
vya michezo.
 | 
Post a Comment