SIKU chache
baada ya Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Mbeya (RCC) kupitisha jina la uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Songwe kuitwa jina la Jakaya Kikwete, Mamlaka ya Viwanja
vya ndege nchini imetoa tamko juu ya mchakato wa ubadilishwaji wa jina unavyokuwa na kusema kuwa jina la uwanja wa ndege wa Kimataifa halibadilishwi
kiholela.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege nchini Bw. Suleiman Suleiman aliyekuwepo
katika ziara ya Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeulizwa kuhusu
kubadilishwa kwa jina la Songwe
International Airport(SIA) na kuitwa jina la Jakaya Kikwete International
Airport.
‘’Jina hili
la SIA lipo katika ramani ya majina ya Viwanja vya ndege duniani, kubadilishwa
jina ni hatua nyingine inayohitaji mchakato wa muda mrefu, kwa sasa tunadeal na
ujenzi wa Uwanja wa ndege suala la jina si la msingi kwetu’’alisema.
Alisema kuwa
vipo viwanja vingi vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege nchini
ambapo majina yao huratibiwa na kuingizwa katika mchakato wa siku 56 na
kulipitisha kimataifa na kwamba jina hili la SIA lilifanyia taratibu zote na
kutambulika kimataifa kwa namba HTGW.
Bw. Suleiman
alisema kuwa kwa kutumia namba hiyo rubani yoyote duniani anajua anatua katika
uwanja gani na kuwa ubadilishaji wa jina wa ghafla unaweza kugharimu utendaji
wa Mamlaka kimataifa.
‘’Rubani
yoyote duniani anajua jina la Songwe baada ya kujitambulisha kimataifa, kwa
sasa tunaendelea kuboresha viwanja vyote vya ndege nchini ili viulingane na
hadhi ya kimataifa,’’alisema Bw. Suleiman.
Kwa upande
wake Waziri wa Uchukuzi Dkt. Mwakyembe aliwataka wananchi na wakazi wa mkoa wa
Mbeya kutumia fursa ya kuwepo kwa uwanja huo kwa kujiinua kiuchumi ikiwa ni
pamoja na kuzalisha mazao ya biashara na chakula katika ubora wa kimataifa.
Dkt.
Mwakyembe ambaye pia alitumia fursa hiyo kutoa mifuko 100 ya saruji katika
shule ya msingi ya Ikumbi iliyopo karibu na uwanja huo ambayo ilitolewa na
kampuni ya db Shapriya inayojenga maegesho uwanjani hapo.
|
Post a Comment
Post a Comment