Ads (728x90)

MTOTO Joseph Dotto(14) AKITOLEWA KATIKA CHASES YA BUS LA KAMPUNI YA MOHAMED TRANS LENYE NAMBA ZA USAJILI T 433 BNG KATIKA STENDI YA MABASI YA MJINI DODOMA.

MTOTO HUYU ALISAFIRI TAKRIBAN UMBALI WA KILOMITA 500 KUTOKEA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAKO ALIAMUA KUTUMIA NJIA HIYO YA MKATO KUSAFIRI KUTOKANA NA KUKOSA NAULI, ALIKUWA AKIELEKEA KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

MTOTO JOSEPH AKIZONGWA NA BAADHI YA WAPIGA DEBE WA STENDI KUU YA DODOMA HUKU WENGINE WAKIMSIFIA KWA UJASIRI WAKE WA KUSAFIRI CHINI YA MVUNGU WA BASI HILO KWA UMBALI MREFU

MTOTO JOSEPH DOTTO ALIYESAFIRI CHINI YA CHASES YA BASI KUTOKA DAR HADI DOM

KWA MUJIBU WA MAELEZO YA DOGO HUYU NI KWAMBA ALIISHI JIJINI DAR AKIWA NA WENZIE WAWILI AMBAO WALIKUWA WAKIFANYA KAZI YA KUOKOTA MAKOPO NA KUUZA NA KISHA KULALA KATIKA STENDI KUU YA MABASI YA UBUNGO LAKINI BAADA YA KUONA HALI YA MAISHA NI NGUMU ALIAMUA KUONDOKA NA KURUDI NYUMBANI KWA KUTUMIA NJIA HIYO AMBAYO NDIYO WALIYOITUMIA WAKATI WAKIENDA JIJINI DAR ES SALAAM






NI KAMA ANAAMBIWA HIVI:,'' WEWE NI KAMANDA HAKUNA MWENYE UWEO KAMA WAKO KUSAFIRI CHINI YA MVUNGU WA BASI''




HIYO NDIYO LIFE DOGO GANGAMALA!!!

MTOTO JOSEPH DOTTO AKIKATIZA MITAA YA MJINI DODOMA MARA BAADA YA KUSHUKA KUTOKA KATIKA BASI HILO, SAFARI YAKE ILIKUWA NI KUELEKEA KAHAMA SHINYANGA AMBAKO NDIKO KIJIJINI

PAPARAZI DOTTO MWAIBALE AKICHUKUA MAWILI MATATU KUTOKA KWA DOGO HUYU AMBAYE ALIFANYA MAAJABU YA AINA YAKE KUSAFIRI CHINI YA MVUNGU WA GARI.

Post a Comment

Post a Comment