SERIKALI
imesema kuwa imeshindwa kuongeza kima cha chini cha Mshahara kutokana na mapato
ya ndani kutokidhi mahitaji ya mishahara yote ya wafanyakazi nchini ambayo ni
asilimia 44 ya bajeti nzima ya nchi ambayo ni zaidi ya sh. Trilioni 10.
Akizungumza
katika kilele cha maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kitaifa mkoani Mbeya
Rais Jakaya Kikwete alisema kuwa bajeti nzima ya mishahara ya wafanyakazi
nchini ni sh. Trilioni 4.7.
Alisema kuwa
bajeti ya serikali ni finyu ambayo haikidhi ongezeko la mishahara ya
wafanyakazi wote nchini na kwamba kiasi
hicho ni sehemu ya bajeti nzima ya serikali kwa mwaka wa fedha.
‘’Hatuwezi
kutumia mapato yote ya serikali kwa mishahara, sio kwamba tunashindwa kuongeza
mishahara kwa ‘’mtima nyongo’’ (roho mbaya) bali uwezo wetu ni mdogo,’’alisema
Rais.
Alifafanua
kuwa mwelekeo wa uchumi wan chi yetu ndio unaotoa tafsiri na kwamba hata hivyo
serikali iko tayari kukaa chini na wafanyakazi kwa nia ya kuzungumza nao
kuangalia kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuweka punguzo la kodi.
Kadhalika
alisema kuwa imeamua kuubeba mzigo kw amalipo ya pensheni ya wafanyakazi nyuma
ya mwaka 1999 ambao wakati sheria hii inaanza serikali ilikuwa bado haijaanza
kuwajibika juu malipo ya pensheni za wastaafu wa serikali.
‘’Kabla ya
mwaka 1999 pensheni za wafanyakazi zilikuwa bado hazijaanza kukusanywa,lakini
serikali italazimika kuchangia waliotakiwa kuchangiwa kabla ya mwaka huo,
tutachangia kwa miaka kumi, mwaka huu tutachangia sh. Bilioni 50,’’alisema na
kuongeza.
‘’Hakuna
mfanyakazi yoyote wa serikali aliyestaafu atakayeshindwa kulipwa mafao yake,’’alifafanua.
Pia Rais
Kikwete aliwaonya waajiri kutowalazimisha wafanyakazi kujiunga kwenye mifuko ya
kijamii kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuwalazimisha kuingia katika mifuko
ambayo haina tija kwa maslahi yao.
‘’Waajiri
acheni tabia za kuwalazimisha wafanyakazi wajiunge kwenye mifuko Fulani yenye
maslahi zenu,hiyo sio tabia nzuri, waacheni wafanyakazi waamue wenyewe,’’
Katika
kuhakikisha serikali inafuatilia kwa karibu masuala ya wafanyakazi Rais Kikwete
alisema kuwa serikali imeweka utaratibu wa kukutana na viongozi wa wafanyakazi
kwa mwaka mara tatu ambapo katika mazungumzo hujadili mustakabali wa
wafanyakazi na maslahi yao.
‘’Wanaozungumza
hawagombani, tutaendelea kuzungumza na kukutana mara tatu kwa mwaka ili
kujadili matatizo yanayoikumba sekta ya wafanyakazi nchini,’’alisema .
Alisema kuwa
serikali itaunda chombo chini ya Ofisi ya Rais kuangalia sekta sita kwa wakati
tofauti kama vile kilimo, biashara, viwanda na mambo mengine yanayoigusa jamii.
Pia alisema
kuwa serikali imedhamiria kuongeza ajira kupitia fursa za uwekezaji ambapo
katika programu hii ajira 195,000 ambapo kati ya hizo 142,000 inatokana na
miradi ya maendeleo na 56,000 kupitia sekta ya umma na kwamba bado kuna fursa
ya kuongeza ajira 600,000.
Alisema kuwa
viongozi wa ngazi za serikali katika maeneo ya mikoa na wilaya wanatakiwa kuwa
wepesi kutenga maeneo ya kuwasaidia vijana ambapo pia kila atakayekopeshwa
anatakiwa kusimamiwa vizuri.
Aidha Rais Kikwete
fursa hiyo ya maadhimisho ya Mei Mosi kusisitiza suala la amani na utulivu wa
nchi na kuwaonya wanaotumia masuala ya udini na ukabila kuacha mara moja kwani
wanaweza kuliingiza Taifa katika maangamizi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
‘’Ndugu
zangu chuki hizi za udini zimetoka wapi, haya mambo yalipoanza wala
hapajulikani, masuala ya mauaji ya
viongozi wa kidini, migogoro ya uchinjaji, hii imeanzia wapi, kabla ya hapa
hatukuwahi kusikia hali hii,’’alisisitiza.
Alisema kuwa
mifumo iliyopo kuhusu suala la uchinjaji imeanza tangu enzi za kale na kwamba
ijapokuwa haijawahi kutungiwa sheria lakini haijawahi kutokea kuwagawa
Watanzania.
Alisema hali
inapobadilika inaonekana na kwamba jambo la muhimu ni kushikilia yanayojenga
badala yanayosababisha chuki na fitina miongoni mwa Watanzania.
‘’Amani
inapovunjika si rahisi kurejea tena hatupaswi kuichezea, tusiwasikilize
wanaotaka kutupeleka pabaya, vita vya
dini havina mshindi, kila mtu anaamini akifia dini yake atakaa kulia kwa
Bwana,’’alisema.
Aliwataja
viongozi wa dini kuketi pamoja na kuangalia namna ya kuondoa matatizo hayo
ambayo yanaweza kuliingiza Taifa katika majanga, ‘’ tumekaa na viongozi wa
kiislamu na kikristo tumeulizana tumepata jibu, mwelekeo uliokuwepo ulikuwa ni
mbaya ambao hauna maslahi kwa Wakristo wala kwa waislamu,’’alisema.
|
Post a Comment
Post a Comment