Ads (728x90)

MMOJA  WA WAJUMBE WA KAMATI ILIYOUNDWA NA NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI AKIAHIDI KUFANYA KAZI KWA UADILIFU KUFUATILIA TUHUMA ZA WIZI WA FEDHA ZA UAKARABATI WA SHULE


KAMATI YA WATU WATANO ILIYOUNDWA NA BW. MULUGO KUFUATILIA WIZI WA SH.500,000 UNAODWIA KUFANYWA NA MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI MUHEZA


 
 
 
STORI NA RASHID MKWINDA-CHUNYA
MWALIMU Mkuu wa shule ya msingi Muheza iliyopo kata ya Namkukwe wilayani Chunya Simiton Kaponda anatafutwa kutokana na madai ya kutafuna jumla ya shilingi 500,000 ambazo zilitolewa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kukarabati majengo ya shule hiyo.

Akizungummza katika mkutano wa hadhara kijijini hapo Bw.Mulugo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songwe alisema kuwa alikabidhi jumla ya shilingi milioni 5 kwa shule kadhaa za jimbo la Songwe na shule hiyo aliipa sh.500,000.

Alisema kuwa hata hivyo tangu atoe fedha hizo hakuna kilichofanyika shuleni hapo ambapo wananchi walidai kuwa Mwalimu huyo ametafuna fedha hizo.


Baada ya taarifa za ubadhirifu huo Bw. Mulugo aliagiza kutafutwa kwa Mwalimu huyo ili atoe maelezo ya kina juu ya namna ambavyo fedha hizo zimetumika lakini hata hivyo hakutokea ndipo Bw. Mulugo alipoamua kuagiza kutafutwa kwa mwalimu huyo ili atoe maelezo ya fedha hizo.

Hata hivyo Mwalimu huyo hakutokea katika mkutano huo na kudaiwa kuwa alikuwa amejificha ndipo Bw. Mulugo alipoamua kuunda kamati ya watu watano kufuatilia tuhuma hizo na kutoa jibu baada ya siku mbili.

Post a Comment