Ads (728x90)

Jengo la CWT ambalo ni refu kuliko yote Jijini Mbeya ambalo limezinduliwa Lift jana
Katibu Mkuu wa CWT Yahya Msulwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Lifti ya Jengo la CWT Mkoa wa Mbeya jana
Hapa ndipo Lifti ya Jengo hilo la ghorofa sita inapoanzia, kila tripu moja inaruhusu watu wasiozidi sab kupanda na kushuka ghorofani
Katibu Mkuu wa CWT Yahya Msulwa akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya, Nyasebwa Chimagu na baadhi ya viongozi wa CWT mikoa ya Nyanda za Juu Kusini


Uzinduzi wa Lifti ya jengo la Chama Cha Walimu mkoani Mbeya (CWT) umeibua gumzo kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na vitongoji vyake huku baadhi yao wakiweka mijadala yao katika mitandao ya kijamii wakielezea hisia zao tofauti.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa zilizopo Mkoa wa Mbeya haujawahi kumiliki jengo refu zaidi ya ghorofa nne ambapo Jengo hilo la ghorofa sita linaelezwa kuwa limevunja rekodi.
Mbali na jengo hilo kuwa ni la kipekee ndani ya Jiji la Mbeya hakuna jengo lolote lililowahi kuwekwa Lifti ya kuwawezesha watumiaji wenye maumbile tofauti, wakiwemo wenye ulemavu na wazee kuweza kupanda ghorofani na kupatiwa huduma.

Katika uzinduzi huo wa kihistoria viongozi mbalimbali wa serikali na wale wa chama cha walimu CWT walihudhuria na kuifanya siku hiyo kuwa ni ya kipekee na ya aina yake katika historia ya Mkoa wa Mbeya tangu dunia iumbwe.
''Huu ndio ukweli hakujwahi kuwa na jengo refu la aina hiyo tangu dunia iumbwe, hili ndilo jengo la kwanza refu na hii ndiyo Lifti ya kwanza kuwepo mkoani Mbeya tangu Mungu aumbe dunia,''alisema mkazi wa Jiji la Mbeya ambaye hujishughulisha na kazi za kupiga Brashi viatu.


Post a Comment