KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LILIAZIMIA
KUWAPELEKA WABUNGE WAKE KATIKA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT KWA NIA YA
KUWAJENGEA UZALENDO NA UKAKAMAVU
,WABUNGE KADHAA HUSUSANI VIJANA
WALIJITOKEZA KUJIUNGA NA JESHI HILO KWA HIARI AMBAKO HUKO WALIKUTANA NA DHARUBA
ZA KIJESHI. WABUNGE HAO MARA WALIPOFIKA KAMBINI WALIKARIBISHWA KWA KUNYOLEWA
NYWELE ZAO, WENGINE WALIKUWA NA RASTA,
NA BAADHI YAO WALIKUWA WAMETENGENEZA NYWELE
ZAO KWA GHARAMA KUBWA, LAKINI WALICHOKUTANA NACHO HUKU HAWAKUKITARAJIA,
MARA BAADA YA KUNYOLEWA NYWELE WOTE
WALIPELEKWA KUPIMWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI, TENA BILA HATA KUPEWA USHAURI HALI
AMBAYO ILILETA TAHARUKI BAINA YAO KWANI WENGI WAO WALIKUWA WAMEPIMA UKIMWI KATI
YA MWAKA MMOJA NA MIEZI KADHAA ILIYOPITA HIVYO KUWAJENGEA HOFU.
HATA HIVYO KUPATA KWAO MAFUNZO
KUMEWASAIDIA NA KUWAJENGEA UZALENDO NA NCHI YAO NA HATA KUWA WAKAKAMAVU.
|
Post a Comment
Post a Comment