WASANII
WA SANAA YA UIGIZAJI MKOANI MBEYA WAMEKUTANA NA KUUNDA SHIRIKISHO LA UIGIZAJI
MKOA WA MBEYA KWA NIA YA KUBORESHA KAZI ZAO ZA SANAA AMBAZO KWA MIAKA MINGI
ZIMEKUWA HAZIWANUFAISHI WAIGIZAJI WENYEWE.
WAIGIZAJI
HAO WAPATAO 234 WALIKUTANA LEO MCHANA KATIKA UWANJA WA CITY PUB ULIOPO MAFIAT
JIJINI MBEYA NA KUELEZEA CHANGAMOTO MBALIMBALI WANAZOKUTANA IKIWA NI PAMOJA NA
KAZI ZAO KUTOTHAMINIWA NDANI NA NJE YA NCHI.AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO HICHO
KATIBU WAQ MUDA WA SHIRIKISHO HILO SADY MWANG'ONDA ALISEMA KUWA VIPAJI VYA KAZI
ZA SANAA VINAKUFA MIONGONI MWA WAIGIZAJI HAO KUTOKANA NA KAZI HIZO
KUTOJULIKANA.
ALISEMA
KUWA WAIGIZAJI WENGI WA MKOA WA MBEYA WANARIDHIKA KUONA KAZI ZAO MAJUMBANI MWAO
BADALA YA KUZITANGAZA KWA JAMII ILI ZITOE MAFUNDISHO KWA JAMII NA KUJIONGEZEA
KIPATO.ALISEMA KUWA KAZI YA UIGIZAJI NI SAWA NA KAZI NYINGINE HIVYO INATAKIWA
KUFANYWA KWA WELEDI NA UMAKINI KWA KUZINGATIA KIPAJI NA ELIMU.
MWANG'ONDA
ALISEMA KUWA WAIGIZAJI WENGI HAWANUFAIKI NA KAZI ZAO HUKU WENGINE WAKIJIKUTA
WAKIIGA KAZI ZILIZOIGIZWA MIAKA MINGI KUTOKANA NA WAIGIZAJI HAO KUTOKUWA
WABUNIFU.
ALISEMA
KUWA ILI KUBORESHA KAZI ZA UIGIZAJI KUNAHITAJI USHIRIKIANO BAINA YA
WAIGIZAJI,MADIRECTOR NA MAPRODYUZA NA KWAMBA NI VYEMA KWA SASA WAIGIZAJI WA
MKOA WA MBEYA WAKATUMIA FURSA YA MKOA WAO KUFANYA KAZI ZINAZOKUBALIKA KATIKA
JAMII NA TAIFA KWA UJUMLA.
ALIFAFANUA
KUWA MKOA WA MBEYA UNA FURSA NYINGI ZA VIPAJI KWA WASANII AMBAO WAKITUMIA VYEMA
VIPAJI NA FURSA ZILIZOPO, MKOA WA MBEYA UNAWEZA KUWA NI SEHEMU YA KIVUTIO KWA
KAZI ZA UIGIZAJI ZITAKAZOTOKEA MKOANI HUMO.
STORI NA
RASHID MKWINDA
|
Post a Comment
Post a Comment