Ads (728x90)

BAADHI YA WAKAZI WA KIJIJI CHA KING'ORI WAKIGOMBEA MAFUTA KUTOKA KATIKA TENKI LILILOANGUKA ENEO HILO.

BAADHI YAO WALILAZIMIKA KUCHOTA MAFUTA KWA MIKONO NA KUWEKA KATIKA MAGUDURIA YAO KWA WAKIWEMO AKINA MAMA NA WATOTO

HAPA KILA MMOJA AKIJITAHIDI KUCHOTA MAFUTA YALIYOMWAGIKA CHINI, MWENYE KIKOMBE!! MWENYE KIJIKO!! ILIMRADI KILA MTU ALIJITAHIDI KWA NAMNA YAKE KUJIPATIA MAFUTA HAYO







LORI AINA YA SCANIA AMBALO LILIANGUKA NA TENKI LAKE KUVUJA MAFUTA


MABASI YAKIJARIBU KUPITA BAADA YA KUSIMAMA KWA MUDA MREFU KUTOKANA NA NJIA HIYO KUZIBWA


MSEMO WA KUFA KUFAANA ULIDHIHIRIKA JANA MAJIRA YA SAA MOJA NA NUSU KATIKA KIJIJI CHA KING’ORI KILOMITA 5 KUTOKA JIJINI ARUSHA BAADA YA LORI  LENYE NAMBA ZA USAJILI T 284 AZG KUANGUKA NA KUMWAGA MAFUTA YALIYOMO KATIKA MATENKI YA GARI HILO NA KUSABABISHA WANANCHI WA KIJIJI HICHO KUGOMBEA MAFUTA HAYO KILA MMOJA AKIWA NA CHOMBO CHAKE.
BILA KUJALI HATARI AMBAYO INGEWEZA KUTOKEA KILA MKAZI WA KIJIJI KILE WAKIWEMO AKINA MAMA,WATOTO VIJANA NA WAZEE WALIMIMINIKA ENEO HILO NA KUCHOTA MAFUTA HAYO MITHILI YA WATU WALIOKUWA WAKICHOTA MAJI KISIMANI.
WANANCHI HAO WALIONEKANA WAKIWA WAMEBEBA MAGUDURIA MAKUBWA NA MADOGO KILA MMOJA KULINGANA NA UWEZO WAKE NA KUKINGA MAFUTA HAYO KATIKA AMOJA YA TENKI LILILOKUWA LIKIBUBUJIKA MAFUTA KWA WINGI HUKU BAADHI YAO WAKIONEKANA WAKICHOTA YALIYOMWAGIKA CHINI KWA MIKONO NA BAADHI YAO KWA VIKOMBE.
AIDHA TUKIO HILO LILISABABISHA MSONGAMANO MKUBWA WA MAGARI YALIYOKUWA YAKIELEKEA ARUSHA NA YALE YALIYOKUWA YAKITOKA ARUSHA KUELEKEA MIKOA MINGINE BAADA YA BASI AINA LA DAR EXPRESS LENYE NAMBA ZA USAJILI T 152 BDQ KUTAKA KUPITA ENEO HILO NA BAADAYE KUSHINDWA BAADA YA KUTELEZA KWENYE MAFUTA NA KUZUIA KABISA NJIA.
KADRI MUDA ULIVYOZIDI KUENDELEA NDIVYO AMBAVYO UMATI WA WATU WALIENDELEA KUMIMINIKA ENEO HILO AMBAPO HATA BAADHI YA WENYE MAGARI WALILAZIMIKA KUSHUKA NA MAGUDURIA KUKINGA MAFUTA HAYO KWA AJILI YA MATUMIZI YA MAGARI YAO.

Post a Comment

Post a Comment