Askari Polisi wakimrejesha rumande Bosi Mmalawi Evance Mwale anayeshitakiwa kwa makosa ya Rushwa ya Ngono |
Na, Bloga Wetu, Mbeya
MENEJA wa Bandari Kavu ya Malawi ‘Malawi Cargo’iliyopo eneo la Iyunga jijini Mbeya Evance Mwale (49)amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya Mbeya akituhumiwa kwa makosa ya kulazimisha ngono kwa mke wa mfanyakazi wake na kutumia vibaya madaraka ya kazi yake.
Mshitakiwa
ambaye ni raia wa nchi jirani ya Malawi alidaiwa kutenda makosa hayo kati ya
Novemba na April mwaka huu katika eneo la Iyunga jijini Mbeya ambapo
alimlazimisha mke wa mfanyakazi wake kufanya naye ngono bila ridhaa yake.
Akisoma
mashtaka ya mshitakiwa huyo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Bw.
Gilbert Ndeuruo,Wakili wa serikali Bw. Basilius Namkambe alisema kuwa
mshitakiwa anakabiliwa mbili za rushwa
ya ngono
na kutumia vibaya madaraka yake.
Bw. Namkambe
alisema kuwa mshitakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo April 11 mwaka huu katika
Hotel ya Moja One iliyopo Iyunga jijini Mbeya ambapo alijaribu kumlazimisha mke
wa mfanyakazi wake Bw.Charles Nyondo, Bi.Roda Kanjeli kufanya naye ngono bila
ridhaa yake.
Alisema kuwa
mshitakiwa alifanya makosa hayo kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano kifungu
namba 25 cha sheria za kuzuia na kupambana na rushwa ACT namba 11 ya mwaka
2007.
Alisema kuwa
shitaka la pili linalomkabili mshitakiwa huyo ni kutumia wadhifa wake wa kazi
kumshawishi Bi. Roda Kanjeli kufanya naye ngono bila ridhaa yake kinyume cha
sheria za kuzuia na kupambana na rushwa namba 31 ACT namba 11 ya mwaka 2007.
Mshitakiwa
ambaye amekana mashitaka yake alirejeshwa rumande hadi Julai mosi mwaka huu baada ya kushindwa
kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye mali
zisizohamishika zenye thamani ya sh. milioni 10 kila mmoja na kukabidhi hati ya
kusafiria mahakamani.
Post a Comment
Post a Comment