MGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHADEMA CHARLES CHANGANI MKELA AMEIBUKA KIDEDEA KWA KURA 1,918 BAADA YA KUMSHINDA MPINZANI WAKE WA KARIBU ALIYEPEPERUSHA BENDERA YA CCM RICHARD SHANGVI ALIYEPATA JUMLA YA KURA 1,163.
AKITANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI HUO JANA SAA 2:00 USIKU MBELE YA LANGO LA CHUO CHA UHASIBU (TIA) JIJINI MBEYA, MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI HUO BI.SAFI ALMASI ALIWATAJA WAGOMBEA WENGINE NA KURA NA VYAMA VYAO KWENYE MABANO KUWA NI AMOSI MWAMBAGI (DP)(20) NA KAPAGA MWAKIBETE (NCCR-MAGEUZI)(17).
BI. ALMASI ALISEMA KUWA JUMLA YA WAKAZI WALIOJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUPIGIA KURA NI 14,576 AMBAPO WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA NI WAKAZI 3,142 NA KURA 24 ZILIHARIBIKA.
AWALI KABLA YA KUTANGAZWA KWA MSHINDI ASKARI WA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA WAKIWA KATIKA MAGARI NA PIKIPIKI WALIANDAMANA KUELEKEA KATIKA ENEO LA UCHAGUZI HALI AMBAYO ILIJENGA HOFU MIONGONI MWA WANANCHI WA MAENEO HAYO LAKINI HATA HIVYO ASKARI HAO WALIFIKA ENEO LA VIWANJA AMBAVYO WALIKUSANYIKA WANANCHI NA KUSIMAMA PEMBENI WAKIANGALIA KINACHOENDELEA.
BAADAYE VIONGOZI WA CHADEMA AKIWEMO MBUNGE WA JIMBO HILO JOSEPH MBILINYI, ALIWATANGAZIA WAFUASI WALIOKUSANYIKA MAENEO HAYO KUTAWANYIKA KUTOKANA NA HOFU YA USALAMA WAO KUFUATIA TUKIO LA BOMU LILILOSABABISHA MAUAJI JIJINI ARUSHA WAKATI WA KAMPENI ZA CHAMA HICHO
MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI MDOGO WA IYELA BI. SAFI ALMASI AKITANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA KATA YA IYELA AMBAPO MGOMBEA WA CHADEMA ALIPATA USHINDI |
ASKARI WA KUTULIZA GHASIA WALIKUWEPO KUANGALIA USALAMA WA ENEO LA UCHAGUZI |
BAADHI YA WAFUASI WA CHADEMA WAKIFUATILIA ALAMA ZA KURA KAMA WALIVYOZIKUTA KATIKA BAADHI YA VITUO VYA KUHESABIA KABLA YA KUTANGAZWA KWA MSHINDI |
BAADHI YA WAFUASI WA CHADEMA WAKISHEREHEKEA USHINDI WA UDIWANI KATA YA IYELA |
Post a Comment
Post a Comment