Ads (728x90)

KUTOKA KUSHOTO NI OFISA HABARI WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ELIAS MHEGERA AKIWA NA MRATIBU WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ONESMO OLENGURUMWA WAKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA MBEYA  KWENYE OFISI YA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI LEO ASUBUHI, KULIA NI MAKAMU MWENYEKITIN WA MBPC MODESTUS NKULU LEO ASUBUHI,

BAADHI YA WANAHABARI NA WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI TAARIFA KUTOKA KWA MAOFISA WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU




MRATIBU WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ONESMO OLENGURUMWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWENYE OFISI YA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA
 

BAADHI YA WANAHABARI WANACHAMA WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA MAOFISA WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU








MTANDAO  WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA UMETOA SOMO KWA WANAHABARI MKOANI MBEYA KUJITAHIDI KUKABILIANA NA MAZINGIRA HATARISHI  YA UITENDAJI KAZI KWA KUJIHAMI KABLA YA KUKUTWA NA MATATIZO AU MAAFA WAWAPO KAZINI.
AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO MAALUMU KATI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA NA WATETEZI HAO WA HAKI ZA BINADAMU KWENYE OFISI YA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA, MRATIBU WA MTANDAO BW. ONESMO OLE NGURUMWA ALISEMA KUWA WANAHABARI WANATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA UTENDAJI WAO ILI KUEPUKA KUPATA MADHARA.
ALISEMA KUWA ASILIMIA KUBWA YA WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA WANAFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA YANAYOHATARISHA MAISHA YAO KUTOKANA NA MFUMO ULIOPO KATIKA JAMII INAYOWAZUNGUKA NA HIVYO KUSHINDWA KUTEKELEZA WAJIBU WAO IPASAVYO.
BW. OLENGURUMWA ALISEMA KUWA MFUMO WA WAANDISHI WOTE NCHINI UNAFANANA HIVYO NI WAJIBU WAANDISHI WENYEWE KUJIHADHARI NA KUWA MAKINI KATIKA UTEKELEZAJI WAO WA KAZI KWA KILA SIKU.
ALISEMA WANAHABARI NI SEHEMU YA KIUNGO MUHIMU ZA KUTOA TAARIFA ZA MIGOGORO MBALIMBALI YA KIJAMII KAMA VILE MAENEO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI, HAKI ZA WATOTO, UNYANYASAJI WA KIJINSIA PAMOJA NA UFUATILIAJI WA TAARIFA ZA KUTOWAJIBIKA KWA WATENDAJI KATIKA SEKTA ZA IDARA ZA SERIKALI AMBAZO BAADHI YAKE ZINAGUSWA NA MATATIZO YA RUSHWA.
ALISEMA KUTOKANA NA HALI HIYO WANAHABARI WANAPASWA KUJUA KUWA KUNA BAADHI YA WATU WATAGUSWA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE NA HIVYO KUJENGA UADUI MIONGONI MWA MAENEO HAYO AMBAYO YANAHITAJI KUPATIWA UFUMBUZI KWA TAARIFA ZA WANAHABARI.
KWA UPANDE WAKE OFISA HABARI WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU BW. ELIAS MHEGERA ALISEMA KUWA WAKO KATIKA URATIBU WA KUIBUA MATATIZO YANAYOWAKUMBA WANAHABARI KATIKA MAENEO YAO YA KAZI NCHINI AMBAPO MTANDAO UTAANDAA MAFUNZO KWA WANAHABARI ILI KUONGEZA WELEDI  NA UTENDAJI KAZI KWA WANAHABARI NCHINI.
BW. MHEGERA ALISEMA KUWA MAZINGIRA YA WANAHABARI KOTE NCHINI YANASHABIHIANA AMBAPO BAADHI YAO WAMEJIKUTA WAKIWA MAADUI KATIKA JAMII WANAYOISHI KUTOKANA NA UTENDAJI WAO NA HIVYO KUJIKUTA WAKO KATIKA HATARI PAMOJA NA KWAMBA WAO NI SEHEMU YA MSAADA KWA JAMII HIYO.
NAO BAADHI YA WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA WALISEMA KUWA WAMEKUWA WAKIKUTANA NA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA UTENDAJI WAO IKIWEMO KUPIGWA NA KUVUNJIWA VIFAA VYAO VYA KAZI NA HIVYO KUSABABISHA KUVUNJIKA MOYO KATIKA KUHABARISHA UMMA MATUKIO YANAYOJIRI KATIKA JAMII.
WALISEMA KUWA BAADHI YA WANASIASA, JESHI LA POLISI NA WANANCHI WA KAWAIDA WAMEKUWA KIKWAZO KATIKA UTENDAJI WA KAZI AMBAPO WAMETAKA KUWEPO NA MAREKEBISHO YA UPATIKANAJI WA TAARIFA KUTOKANA NA UKIRITIMBA KWA HABARI ZA JESHI LA MAGEREZA, USALAMA WA TAIFA NA MAHAKAMA.


Post a Comment

Post a Comment