NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKISISITIZA JAMBO WAKATI WAUZINDUZI WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO KWENYE VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE JIJINI MBEYA MAPEMA LEO ASUBUHI |
BAADHI YA WAKAZI WA JIJI LA MBEYA WALIOJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MPANGO MPYA WA USAJILI WA UZAZI NA VIFO KATIKA MKAKATI WA USAJILI WA VIZAZI KWA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO |
WATOTO KAMA HAWA WANAHITAJI KUSAJILIWA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA ILI KUWAJENGEA MFUMO MZURI WA MAISHA YAO SIKU ZA USONI |
NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ANGELA KAIRUKI AKIZINDUA RASMI MFUMO MPYA WA USAJILI WA VIZAZI NA VIFO JIJINI MBEYA LEO ASUBUHI |
ASILIMIA 7.7
ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ndio waliosajiliwa na na kupata
vyeti vya kuzaliwa kati ya asilimia 14 ya watoto wote waliozaliwa ikiwa ni asililimia 23 tu ya wananchi wote ambao
wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini.
Kwa mujibu
wa taarifa ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA) katika uzinduzi wa
mfumo mpya wa usajili wa vizazi kwa watoto waliochini ya miaka mitano, ni
kwamba takwimu hizo zimekuwa haziridhishi kwa kutambua umuhimu wa usajili na
Utunzaji wa kumbukumbu muhimu za vizazi mwaka 2011.
Akizungumza
katika uzinduzi wa mfumo mpya wa usajili kwa watoto waliochini ya miaka mitano kwenye
viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA)Bw. Vicent Mrisho alisema kudorora kwa
mfumo wa usajili kumechangia serikali kukosa takwimu muhimu kwa mipango ya maendeleo ya Taifa.
Bw. Mrisho
alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa takwimu zisizoridhisha za kumbukumbu za
vizazi mwaka 2011RITA kwa kushirikiana
na wadau mbalimbali ilibuni mkakati wa usajili wa watoto wa umri wa chini ya
miaka mitano wenye lengo la kuboresha hali ya usajili nchini na kuweka
kipaumbele kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.
Alisema kuwa
kundi hili la watoto chini ya miaka mitano lilichaguliwa kwa sababu ya
kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa
anapata cheti kabla ya kuruhusiwa kurudi nyumbani na pia kundi ambalo
hutumika kama kipimo katika mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za Mtoto na
malengo la Milenia.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Bi. Angela Kairuki ambaye
alimwakilisha Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda alisema mfumo mpya wa usajili ni
sehemu ya ugatuaji wa madaraka kupeleka huduma katika ngazi ya serikali za
mitaa.
Alisema
awali usajili ulikuwa ukifanyika katika ofisi za Mkuu wa wilaya hali ambayo ilichangia
kujitokeza kwa idadi ndogo na hivyo kuleta changamoto inayohitaji mipango
mahsusi na kwamba mkakati huu utatoa suluhisho kwa mpango wa maendeleo ya
Taifa.
Uzinduzi huu
wa usajili wa vizazi na vifo utafanyika katika mikoa mitano ya Mbeya, Mwanza,Simiyu,
Shinyanga na Geita ambapo kwa mkoa wa Mbeya kutakuwa na vituo 333
vya usajili katika ngazi ya ofisi za watendaji wa kata na vituo vya afya.
Post a Comment
Post a Comment