| 
 
WAZIRI
  wa Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa siku tisini kuondolewa matrekta yanayofanyakazi
  bandarini na badala yake yapelekwe vijijini ili yasaidie kufanya shughuli za
  kilimo. 
Dkt.
  Mwakyembe aliyasema hayo leo mchana wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Kilimo
  Nane Nane ambayo yanajumuisha mikoa sita ya nyanda za juu kusini na kufanyika
  Jijini Mbeya. 
Alisema
  kuwa wakulima wamekuwa wakipata shida nyenzo za kilimo ilhali bandarini kuna
  matrekta yanayopakua mizigo kinyume na kazi zake za kilimo.'' 
Kwa
  kuwa hili jambo lipo mikononi mwangu nitalishughulikia ipasavyo, naagiza
  miezi mitatu hadi Oktoba yawe yameondoka pale bandarini''alisema Dkt.
  Mwakyembe.Alisema kuwa atatoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vingine
  vye usalama kuhakikisha matrekta yote yanaenda vijijini badala ya kuzagaa
  mijini kwa kazi ambazo hazina manufaa kwa Mkulima. 
''Nataka
  Matrekta yalime sio kubeba mizigo bandarini,''alisisitiza. 
Aidha
  Dkt. Mwakyembe  aliwataka wakulima kuboresha mbinu za uzalishaji kwa
  kulima kilimo cha kisasa kwa kuwatumia wataalamu ili kuongeza tija na kipato. 
Alisema
  kuwa azma ya uzalishaji inahitaji mazingira yaliyowezesha na kwamba serikali
  imeongeza kasi kuboresha miundo mbinu katika mwaka wa fedha wa 2013 ambapo
  jumla ya sh. Bilioni 162.5 zimetengwa kwa miradi ya umeme kuanzia mwezi
  Oktoba zitakazochochea uanzishwaji wa miradi. 
 
Pia
  Dkt. Mwakyembe alisema kuwa serikali imetenga jumla ya sh.Bilioni 5 kwa ajili
  ya ukarabati wa barabara za vijijini ili kuboresha shughuli za kilimo ambapo
  barabara kuu za kiwango cha lami zinazounganisha mikoa ya Ruvuma, Katavi na
  Rukwa zinaendelea kutengenezwa.  | 
Post a Comment
Post a Comment