Baadhi ya Maimamu wakiwa katika benchi wakifuatilia michezo mbalimbali inayoendelea katika uwanja wa Sokoine wakati wa tamasha la Id el fitri |
Mratibu wa michezo katika tamasha la Id el Fitri Shekhe Ibrahimu Bombo akimpima mmoja wa wazee aliyejitokeza katika mashindano ya kufukuza kuku kwenye uwanja wa Sokoine |
Baadhi ya wazee wakishindana kumfukuza kuku katika mashindano yaliyoandaliwa na Maimamu kwenye Tamasha la Id el fitri uwanja wa Sokoine |
Mmoja wa wazee akiwa amemshika Kuku baada ya kushinda katika mbio za kukimbiza Kuku kwenye Tamasha la Id el Fitri |
Baadhi ya maimamu wa Jiji la Mbeya wakishindana katika mbio za kukimbia kwenye magunia |
Watoto waliojitokeza katika mashindano ya kulishana Icecream huku wakiwa wamefungwa vitambaa usoni |
Vijana naoa walijitokeza katika mashindano ya kufukuza Sungura |
Akina mama nao hawakurudi nyuma walijitokeza katika mashindano ya kukuna nazi kwa speed ya dakika 10 |
Akina Dada nao bila ajizi walijitokeza kwenye mashindano ya kumenya viazi kwa speed |
Maimamu na maamuma nao walishiriki katika mashindano ya kuvuta kamba |
Michezo ya KARATE pia ilikuwepo ambapo vijana walijitokeza kuonesha umahiri waao wa kurusha mateke na kupiga KATA |
Timu ya MADIWANI wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambao walijitokeza kuchuana na maimamu kwenye kabumbu, maimamu walifungwa Bao 2-1 |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Athumani Diwani akisalimiana na timu ya maimamu kabla ya mechi kati yao na madiwani wa halmashauri ya Jiji la Mbeya kwenye tamasha la Id el fitri |
Kamanda wa Polisi Athumani Diwani akimkabidhi zawadi kipa bora wa timu ya Madiwani wa halmashauri ya Jiji la Mbeya |
Post a Comment
Post a Comment