Taarifa ambazo zimezagaaa katika mitandao ya kijamii nchini zimedai kuwa Shekhe Ponda Issa Ponda amepigwa risasi na askari polisi wakati akitoka kwenye mhadhara wa kidini Mjini Morogoro. Taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya kumaliza mkutano Shekhe Ponda alifuatwa na askari polisi ambao walimtaka aingie kwenye Defender ya polisi badala ya teksi aliyokuja nayo, baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu walizuia Shekhe Ponda asiingie katika gari hilo ndipo imedaiwa kuwa Shekhe Ponda aliingia katika teksi aliyokuja nayona kuwaaga waumini kuwa ataenda kuswali katika msikiti maarufu unaoitwa Mungu Mmoja Dini Moja. Inadaiwa kuwa wakati anaondoka katika gari hilo mara gari la Polisi lilisimama mbele ya teksi hiyo na kwa kitendo cha haraka inadaiwa alipigwa risasi mbili na kukimbizwa katika hospitali kuu ya mkoa, na baadaye taarifa zenye utata zinaeleza kuwa kuwa Shekhe huyo amejeruhiwa vibaya ambapo baadhi ya watu wanaeleza kuwa Shekhe huyo amepoteza maisha huku wengine wakieleza kuwa shekhe huyo ni mzima isipokuwa amehifadhiwa sehemu maalumu kwa kuhofia kudhuriwa na watu waliompiga risasi.
Picha juu zinaonesha matukio mbalimbali ya Shekhe Ponda katika mhadhara uliofanyika mjini Morogoro jana jioni kabla ya kudaiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya |
Post a Comment
Post a Comment