TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE”
TAREHE 22. 08. 2013.
WILAYA YA
MBOZI – AJALI YA GARI KUACHA NJIA KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 21.08.2013
MAJIRA YA SAA 15:00 HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA LWATI BARABARA YA
KAMSAMBA /MLOWO WILAYA YA MBOZI MKOA WA MBEYA. GARI T.855 ACJ AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA CLEMENT S/O EXAVERY, LILIACHA NJIA NA
KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA LAUDEN
S/O MWAMPANGALA, MIAKA17, MKULIMA, MNYIHA, MKAZI WA NAMBIZO NA MAJERUHI KWA
WATU TISA WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA
MBOZI MISHENI. CHANZO MWENDO
KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA NAMBIZO.
DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA
MBARALI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 21.08.2013
MAJIRA YA SAA 13:45 HRS HUKO KATIKA
KIJIJI CHA MLANGALI WILAYA YA
MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.901
ASQ/T.415 AXA AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA SHADRACK S/O HAMIS, MIAKA 34, MMAKUA,
MKAZI WA IRINGA LIKITOKEA MBEYA KUELEKEA MAFINGA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MONICA D/O MHAHWA, MIAKA 56, MBENA,
MKAZI WA MAKETE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Post a Comment
Post a Comment