Ads (728x90)

Eneo hili kama linavyoonekana pichani linajitambulisha ni wapi, hapa ndipo panapozalishwa bidhaa za matunda kama vile Tomato Sauce na Chilli Sauce

Pamoja na kuzalishwa bidhaa hizo muhimu za chakula ambazo zinapendwa na walaji wengi nchini lakini mazingira yake yameanza kuwatia kero wapita njia kutokana na harufu kali inayotoka eneo hilo

Nje ya jengo hilo linalozalisha bidhaa hizo kuna ghuba linalovuja maji yenye uvundo kamalinavyoonekana pichani na hivyo kusababisha wapita njia kuziba pua
Pamoja na ghuba hilo kujaa takataka zinazotoa harufu katika kiwanda hicho, hakuna jitihada zozote zinazoonekana kufanywa ili kuondoa kero hiyo kwa wapita njia


Hili ni jengo ambalo ni kiwanda cha miaka mingi kinachozalisha bidhaa za matunda,ambacho kimeonekana kukosa miundo mbinu ya kuhifadhi taka zinazozalishwa na kusababisha harufu kali kwa wapita njia na hivyo kuhatarisha afya za wakazi wa maeneo ya Ipogolo Manispaa ya Iringa

Post a Comment

Post a Comment