Mtungo katika bodaboda katika barabara nyembamba ambayo inakatiza katikati ya mto mrefu wenye mamba wakali |
Hapa wakitafakari namna ya kufika kijijini ambako usafiri wake ni bodaboda kukatiza katika mto wenye mamba |
Barabara nyembamba inayokatiza katika mto mkubwa wenye mamba, hapa jamaa roho juu juu |
Jamaa wamemkumbatia mwendesha bodaboda kuvuka katika barabara nyembamba inayokatisha kwenye mto mkubwa, mwingine akiogopa kupita akiwa amesimama mwanzoni mwa njia nyembamba anaonekana kwa mbaali |
Jamaa walipovuka wakajiona ni mashujaa ilhali walipoikuwa katikati ya mto nusura waloweshe sarawili zao |
Huyu alishindwa uvumilivu akajikaza kiume na kupita kwenye kijinjia huku akitetemeka na kuvuka |
Pamoja na woga wa wageni kupita katika njia hiyo, wenyeji walikuwa wakipita huku wakiwa na shehena ya mizigo kama wanavyoonekana wakazi hawa wa kijiji cha Ngana wakiwa wamebeba mihogo katika baiskeli |
kumalizika kwa safari ilikuwa ni namna ya kutafakari kuupata msosi ghafla wakaivamia mihogo iliyokuwa ikikaangwa kwa mafuta ya mawese kutuliza njaa |
Baada ya kuona njaa inauma sana ilibidi waombe msaada wa kisu ili kujisevia kukatakata kachumbari na kulumangia kwa mihogo |
Post a Comment
Post a Comment