MCHUANO
wa ligi kuu umeendelea leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine
Jijini ambapo wenyeji Mbeya City waliwakaribisha Coastal Union ya Tanga
na kuilazimisha kutoka sare ya bao 1-1.
Mchezo
huo umeanza kwa kuviaziana ambapo timu ya Coastal Union ndiyo ilikuwa
ya kwanza kuliona lango la timu ya Mbeya City dakika
ya saba ya mchezo baada ya mchezaji wa timu ya Coastal Union Haruna
Moshi Boban kuwatoka walinzi wa Mbeya City, Anton Matogolo,Alex Seth na
Steven Mazanda na kujipatia bao kwa mkwaju hafifu uliompita golikipa wa
timu ya Mbeya City David Baruani.
Goli
hilo liliamsha hoihoi kwa washabiki wachache wa timu ya Coastal Union
ambao walikuwa wakiburudisha uwanja kwa ngoma yao ya Mdumange.
Baada
ya goli hilo wachezaji wa timu ya Coastal Union walionesha kupoteza
muda ambapo kila mpira ulipofika katika goli lao golikipa wa timu hiyo
Hassan Shaaban alikuwa akiuchezea chezea kwa muda mrefu bila kuupiga
hali ambayo iliibua malalamiko kwa washabiki ambao walianza kumzomea.
Hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika Coastal Union walitoka kifua mbele kwa
bao 1-0,ambapo hata hivyo Golikipa wa Coastal Union Shaaban alitoka nje
ya uwanja baada ya maumivu ya musuli na badala yake kuingia Said Libawa.
Kipindi
cha pili kilianza kwa mashambulizi makali yaliyofanywa na timu ya Mbeya
City na hivyo kulazimisha kona tatu zilizoelekezwa kwa timu ya Coastal
ambazo hata hivyo hazikuzaa matunda.
Mchezo huo ambao
ulitawaliwa na kipyenga cha mara kwa mara kutoka kwa refarii Oden Mbanga
wa Dar es salaam aliyesaidiwa na washika vibendera Hamis Chang'walu na
Omar Kambangwa kutokana na rafu za hapa na pale.
Mashambulizi
katika lango la timu ya Coastal yalizaa matunda katika dakika za lala
salama ambapo katika dakika ya 89 wachezaji wa timu ya Mbeya City
walionana vizuri na kusababisha goli la kusawazishwa lililofungwa kwa
njia ya kichwa na mchezaji wa timu ya Mbeya City Mwagane Yeya aliyeingia
katika kipindi cha pili.
Hata hivyo dakika chache baadaye
refarii ametoa kadi nyekundu kwa wachezaji wawili wa timu ya Coastal na
Mbeya City ambao
walionekana kubishana uwanjani ambao ni Marcus Ndeheli na Richard Peter
na baadaye zikiwa zimesalia sekunde kadhaa kumalizika kwa mchezo Haruna
Moshi naye alipewa kadi nyekundu kwa kumtolea lugha ya matusi mshika
kibendera Hamis Chang'walu.
Hadi Kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu zilikuwa sare ya bao 1-1. |
Post a Comment
Post a Comment