Gari la Wagonjwa lililombeba Nyenyembe kutoka Uwanja wa Ndege hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili (PICHA KWA HISANI YA FACEBOOK YA KENETHY NGELESI)
.'Ndugu Zangu Waandishi wa Habari na wadau
wengine wa habari nawashukuru kwa maombi na dua zenu, Mwenyezi Mungu
anaendelea kunipa afya njema na ninaendelea na matibabu, leo hii naenda
kufanya check up nipo hapa Muhimbili Hospitali, nashukuru
kwa kunipigia ndugu yangu Rashid, vipi harakati zinaendeleaje huko
Mbeya?
Ni sauti ya Mwandishi wa habari na Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya
Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe alipokuwa
akiongea nami kwa njia ya simu muda mfupi uliopita, nimefarijika kusikia
sauti yake yenye nguvu isiyo na mikwaruzo kama ilivvyokuwa hapo awali,
akizungumza kwa matumaini huku akileta utani wake wa kawaida, ni faraja
kubwa na ni fursa pekee ya kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote ambaye
alipangalo ndilo huwa, Nyenyembe mpiganaji, mwanahabari mkongwe, mshairi
na mchambuzi wa mambo mbalimbali ya kijamii,uchumi na siasa sasa hivi
yupo feet na anaendelea vyema kiafya. |
|
Post a Comment
Post a Comment