| Gari la Wagonjwa lililombeba Nyenyembe kutoka Uwanja wa Ndege hadi Hospitali ya Taifa Muhimbili (PICHA KWA HISANI YA FACEBOOK YA KENETHY NGELESI) 
 .'Ndugu Zangu Waandishi wa Habari na wadau 
wengine wa habari nawashukuru kwa maombi na dua zenu, Mwenyezi Mungu 
anaendelea kunipa afya njema na ninaendelea na matibabu, leo hii naenda 
kufanya check up nipo hapa Muhimbili Hospitali, nashukuru
 kwa kunipigia ndugu yangu Rashid,  vipi harakati zinaendeleaje huko 
Mbeya?
 Ni sauti ya Mwandishi wa habari na Mwenyekiti Mstaafu wa Klabu ya
 Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya Christopher Nyenyembe alipokuwa 
akiongea nami kwa njia ya simu muda mfupi uliopita, nimefarijika kusikia
 sauti yake yenye nguvu isiyo na mikwaruzo kama ilivvyokuwa hapo awali, 
akizungumza kwa matumaini huku akileta utani wake wa kawaida, ni faraja 
kubwa na ni fursa pekee ya kumshukuru Mwenyezi Mungu muweza wa yote ambaye 
alipangalo ndilo huwa, Nyenyembe mpiganaji, mwanahabari mkongwe, mshairi
  na mchambuzi wa mambo mbalimbali ya kijamii,uchumi na siasa sasa hivi 
yupo feet na anaendelea vyema kiafya.
 | 
 | 
Post a Comment