Ads (728x90)

Basi la timu ya Tanzania Prison ambalo linadaiwa kuvunjwa vioo na mashabiki wa timu ya Mbeya City mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya timu hizo, Mbeya City ilishinda bao 2-0

Kioo cha nyuma cha Basi aina ya Coaster lenye namba za usajili MT 0081 mali ya Jeshi la Magereza kikiwa kimevunjwa na watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa Mbeya City.

Mchezaji wa timu ya Tanzania Prison Salum Kimenya akiwa ameumizwa mkono na watu wanaodai kuwa ni mashabiki wa timu ya Mbeya  City.

Mchezaji wa Prison  Ibrahim Mamba ambaye pia anadaiwa kujeruhiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa timu ya Mbeya City.

Kapteni wa timu ya Tanzania Prison Lugano Mwangama ambaye pia anadaiwa kupigwa shingoni na watu waliolishambulia Basi la timu yao mara baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na Mbeya City.

BARUA YA TANZANIA PRISON KWA UONGOZI WA TFF JUU YA MALALAMIKO YAO KUHUSU MCHEZO WAO NA MBEYA CITY

Wachezaji wa Tanzania Prison waliojeruhiwa

Katibu wa Chama Cha Mpira mkoa wa Mbeya Suleiman Haroub akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo asubuhi juu ya tukio la vurugu za mashabiki katika mechi kati ya Mbeya City na Prison zote za Mbeya.

Gari aina ya Corolla ambalo linadaiwa kuharibiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa timu ya Prison.

Mmoja wa mashabiki wa timu ya Mbeya City Simon Mwakatobe akielezea namna ambavyo wachezaji wa timu ya Prison walivyoshuka kwenye gari lao na kuanza kurusha mawe kwa mashabiki wa Mbeya City.


Mshabiki wa timu ya Mbeya City Furaha Sankey naye akielezea namna ambavyo wachezaji wa Prison walivyoanza kuwarushia mawe mashabiki wa Mbeya City.
Mwenyekiti wa timu ya Mbeya City tawi la Mwanjelwa Willy Mastala akionesha jeraha lililotokana na kupigwa na askari polisi wakati wa vurugu mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Mbeya City na Prison.

Willy Mastala akionesha jeraha la kirungu alichopigwa na askari polisi mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Mbeya City na Prison.

Mwenyekiti wa Mbeya City tawi la Mwanjelwa, Willy Mastala


Gari la timu ya Tanzania Prison linavyoonekana kwa mbele

Gari la timu ya Prison linavyoonekana mara baada ya kuvunjwa vioo na watu wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa Mbeya City.

Gari aina ya Coaster mali ya Jeshi la Magereza ambalo limevunjwa kioo cha nyuma na watu wanaosadikiwa kuwa ni mashabiki wa timu ya Mbeya City mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu kati ya timu hizo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jana.

Post a Comment

Post a Comment