Moja ya nyumba zinazodaiwa kuwa ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambazo zinamilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara |
Nyumba ya Halmashauri ya wilaya ya Mbozi ambayo imepangishwa kwa taasisi ya kifedha ambayo inadaiwa kuwa fedha zinazotokana na pango la nyumba hiyo haziingii katika mfuko wa Halmashauri ya wilaya |
Jengo la Halmashauri ya wilaya ambayo ni sehemu ya kitega uchumi cha halmashauri hiyo mapato yatokanayo na pango la nyumba hiyo yanadaiwa kuwa hayaingii kwenye mfuko wa halmashauri ya wilaya. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Elick Ambakisye akizungumza katika kikao cha Halmashauri ya wilaya ya Mbozi na kutoa tamko la kuvunja mikataba kwa wapangaji wa halmashauri hiyo |
Baadhi ya Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakifuatilia kwa makini kikao cha Baraza ambacho kilitoa tamko la kuvunjwa kwa mikataba ya nyumba kwa wapangaji wake |
HALMASHAURI
ya wilaya ya Mbozi imezinduka na kuvunja mikataba ya baadhi ya nyumba zake
ambazo ilizitelekeza kwa zaidi ya miaka 30 na kuwataka wamiliki wa nyumba hizo
kukabidhi nyaraka za mikataba walioingia na watumishi wa halmashauri hizo.
Akizungumza
katika kikao cha Baraza la Madiwani wa wilaya ya Mbozi Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Elick Ambakisye alisema kuwa,baada ya kufuatilia kwa kina
imebaini kuwa wapo watendaji wa halmashauri walioingia mikataba na wapangaji wa
nyumba hizo ambazo halmashauri ilikuwa haipati chochote.
Alisema kuwa
kuanzia jana Novemba Mosi nyumba zote za halmashauri ambazo upangaji wake una
utata mikataba yake itavunjwa na kupitiwa upya ili halmashauri ianze kunufaika
na mali zake.
Bw.
Ambakisye alisema kuwa imebainika kuwa nyumba tatu zilizoripotiwa ni mali ya
halmashauri ambapo aidha wapangaji wake waliingia mkataba na watendaji wa awali
ambao hawakuweka bayana mikataba ya mali za halmashauri hiyo.
Alizitaja
nyumba hizo kuwa ni pamoja na MDC ambayo ni Bar iliyokuwa ikimilikiwa na
halmashauri lakini kutokana na kushindwa kuiendesha ilitelekezwa kwa
wafanyakazi ambao walikusanya fedha za mapato ya Bar hiyo bila kuwasilisha
ofisini.
Alisema
nyumba nyingine ni jengo ambalo limepangishwa duka la Tanganyika Farmers
Association (TFA) ambalo waliingia mkataba na halmashauri kwa miaka 12 na
kwamba mkataba huyo utapitiwa upya na kuanzia Novemba Mosi makusanyo yote ya
kodi yataingia katika mfuko wa halmashauri.
Aidha
aliitaja nyumba nyingine ya halmashauri ambayo ilikabidhiwa kiholela kwa chama
cha Akiba na Mikopo cha akina mama WAT SACCOS ambao baadaye walijimilikisha kiholela ikiwa
ni pamoja na kuingia mkataba na wapangaji wengine na fedha zilizopatikana
zilikuwa zikiingia katika mfuko wa akina mama bila kuihuisha Halmashauri.
Alisema
kuanzia sasa makusanyo ya fedha zote ambazo kwa zaidi ya miaka 30 zimekuwa
zikiingia katika mifuko ya pembeni zitaingia katika mfuko wa Halmashauri ya
wilaya ya Mbozi.
Awali gazeti
hili liliripoti taarifa za kutafunwa kwa mamilioni ya fedha zilizotokana na
nyumba 3 za halmashauri kwa takribani miaka 30 huku ikidaiwa kuwa fedha hizo
zilikuwa zikiingia mifukoni mwa watendaji wachache waliodaiwa kuficha vyanoz
hivyo vya mapato.
Ilidaiwa kuwa tangu
zilipopangishwa nyumba hizo mapato yake yalikuwa hayajulikani huku baadhi ya
watendaji wakidaiwa kutafuna fedha hizo ilhali halmashauri husika ikiwa haiwatambui
wapangaji wa nyumba hizo.
Post a Comment
Post a Comment