Dkt.Sengondo Edmund Mvungi enzi za uhai wake |
Dkt. Mvungi akipelekwa katika chumba cha uangalizi maalum ICU kabla hajahamishiwa katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini |
Taarifa
zilizotujia jioni ya leo zinadai kuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na
Mhadhiri mwandamizi wa sheria Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dkt. Sengondo Edmund
Mvungi amefariki leo katika hospitali ya Milpark nchini Afrika Kusini.
Dkt.Mvungi
ambaye pia aliwahi kugombea Urais kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi mwaka 2005
alivamiwa na kupigwa mapanga na majambazi ambapo baadaye alilazwa katika
hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kitengo cha mifupa MOI na kuwekwa chini ya
uangalizi maalumu (ICU)kabla ya kuhamishiwa nchini Afrika Kusini Novemba 7.
Aidha Jeshi
la Polisi kanda maalum limedai kukamata watuhumiwa 9 wanaodaiwa kukutwa na
mapanga yanayodaiwa kutumika katika uvamizi huo.
Post a Comment
Post a Comment