Gervas Kadaga akiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya baada ya kujeruhiwa na kisu tumboni baada ya kumuua kwa kumchoma kisu mkewe |
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Mahango kata ya Madibila wilayani Mbarali mkoani Mbeya aliyefahamika kwa jina la Jitihada Mamga(20) ameuawa kwa kuchomwa kisu na mumewe aliyefahamika kwa jina Gervas Kadaga(25) ambaye pia ni mkazi wa kijijini hapo.
Tukio hilo
limetokea juzi Novemba 21 majira ya saa 1:00 jioni baada ya kutokea ugomvi
baina ya wapenzi hao ambapo marehemu alikutwa na majeraha tisa ya kisu katika
sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Bw. Diwani Athumani alisema
kuwa marehemu alifia nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa ambaye amelazwa katika
hospitali ya Rufaa Mbeya naye amejeruhiwa kwa kuchomwa na kisu tumboni.
Hata
hivyo Kamanda Athumani alisema kuwa hadi sasa hakijafahamika chanzo halisi cha
ugomvi huo ambapo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku mtuhumiwa akiwa
amewekwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya
alikolazwa.
Tukio la
aina hiyo ni la pili kwa kipindi kisichozidi wiki mbili ambapo Novemba 12
mke na mwanawe wa kiume waliotambulika kwa majina ya Husulina Kornel(42)
na mwanaye Kondo Alphonce Chikondo(19) wakazi wa kijiji cha Iseche kata ya
Mwambani tarafa ya Kwimba wilayani Chunya walishirikiana kumuua mumewe
aliyefahamika kwa jina la Sylvester Chikondo(55).
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Athumani ni kwamba mwanamke
huyo Husulina Kornel aliyedaiwa kushirikiana na mwanaye kumuua mumewe
mumewe alikamatwa Novemba 20 huko Mwambani Chunya.
Kamanda Athumani alisema kuwa katika mahojiano ya Jeshi la
Polisi na mwanamke huyo alidai kuwa alifanya mauaji hayo peke yake bila
kumhusisha mwanaye ambaye anaendelea kutafutwa na Jeshi la Polisi.
Aidha alisema kuwa asilimia kubwa ya matukio ya mauaji ya
aina hiyo yanatokana na migogoro ya ndoa na wivu wa kimapenzi na kwamba ni
vyema wanandoa wakatatua migogoro yao
ya ndani kwa njia ya mazungumzo ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Akizungumza
katika hospitali ya rufaa alikolazwa mama mkubwa wa Gervas aliyejitambulisha
kwa jina la Martha Lugenge alisema kuwa vijana hawa walikutana Madibila kila
mmoja akiwa katika shughuli zake ndipo walipoamua kuishi pamoja.
Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.
Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema.
Alisema yeye alipewa taarifa za tukio hilo siku inayofuata na kwamba alipofika alikuta ndugu wa marehemu wameuchukua mwili wa mtoto wao kwa ajili ya taratibu za mazishi na kwamba hajui chanzo cha ugomvi uliosababisha wapigane visu.
Mama huyo alisema kuwa vijana hao hawajawahi kupata mtoto na kwamba hawajaanza kuishi pamoja muda mrefu; ''Wote ni watoto, kwani wameanza kuishi muda mrefu? wamekutana kila mmoja akiwa katika kazi zake, ndipo walipoanza kuishi kama mke na mume,''alisema.
Kijana Grevas Kadaga anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma kisu akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya alikolazwa kwa ajili ya matibabu |
Mama mkubwa wa Gervas Martha Lugenge akimjulia hali mwanaye katika hospitali ya Rufaa Mbeya |
Gervas Kadaga akiwa katika wodi namba Moja Hospitali ya Rufaa Mbeya |
Post a Comment
Post a Comment