Ads (728x90)

Katibu Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Waziri wa ICT wa Thailand.
Timu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania katika Maonesho ya ITU Telecom World
Timu ya Tanzania ikiwa katika mikakati ya pamoja ili kushiriki kikamilifu mbili zilizosalia,  Hapa wakifanya majumuisho taarifa za  Matukio ya siku ya pili.
Kauli Mbiu ya Tanzania katika Kongano la ITU Telecom.
Na Innocent Mungy - Bangkok Thailand
Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani (ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji la Bangkok nchini Thailand.

Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika Ulimwengu wa TEHAMA, linashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serikali, wanashiriki Kongano hili katika kipindi ambacho mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mawasiliano duniani yanaendelea.

Mabadiliko haya yanamesababisha dunia kuwa na Changamoto ya kuyakubali  na kukabiliana na Changamoto zake kutokana na faida za  mabadiliko kuwa kubwa kwa Jamii ya Habari duniani. Akizungumza jijini Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa amesema Tanzania iko tayari na imeshapokea mabadiliko na imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inapokuwa mabadiliko bila tatizo.

Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu wa mabadiliko ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hususan katika kipindi hiki cha mfumo wa kidijiti kwa kuwa ndiyo njia pekee ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.

Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John Nkoma amesema Tanzania tayari  mstari wa mbele kuhakikisha inachochea mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi wafaidike na huduma za Mawasiliano. 

"Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni za muingiliano wa teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia katika mfumo wa Utangazaji wa digitali na tunaendelea kuweka mazingira mazuri ya kuwepo kwa huduma nyingi zaidi kurahisisha maisha ya watanzania". Amesema Profesa Nkoma.

Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya Afya, Kamisheni ya Sayansi na  Teknolojia,  DTBi ya wavumbuzi na wagunduzi, NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.

Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 - 22 Novemba 2013. Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi "Tanzania: Africa Strategic ICT Hub". Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia TEHAMA. Banda la Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia kujifunza jinsi Tanzania imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na jinsi wananchi wanafaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.

Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa kuchochea zaidi upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano Maalum wa Wawekezaji Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu Katibu Mkuu wa ITU Bwana Houlin Zhao.

Post a Comment

Post a Comment