Kwa
mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi kwa vyombo vya habari iliyotolewa na
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi alisema kuwa tukio hilo limetokea
Januari 10 majira ya saa 3:00 usiku
katika kijiji cha Kapele wilayani humo.
Kamanda
Msangi alisema kuwa chanzo cha mauaji hayo kimetokana na madai kuwa muuaji
ambaye ni ndugu wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Bonny Silumbe alimchoma
kisu mgongoni nduguye Adam kwa madai kuwa alikuwa akilipiza kisasi baada ya
Adam kumtangaza kuwa alimtorosha mke wa mtu.
Alisema
mara baada ya Adam kuchomwa kisu alikimbizwa katika Hospitali wilaya ya Mbozi
kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo Januari 12 majira ya saa 3:30 asubuhi
alifariki dunia.
‘’Chanzo
kinaelezwa kuwa ni kulipiza kisasi, baada ya marehemu kumtangaza mtuhumiwa hapo
kijijini kuwa alimtorosha mke wa mtu, mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio, mwili
wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi,’’alisema
Kamanda Msangi.
Kamanda
Msangi ametoa taarifa kwa umma kuwa yoyote atakayemuona mtuhumiwa atoe taarifa
kituo cha polisi au ajisalimishe mwenyewe kabla ya kutiwa mbaroni na vyombo vya
dola na kwamba wanajamii wanapaswa kutatua matatizo yao ya kifamilia badala ya
kuchukua sheria mkononi na kusababisha madhara.
Wakati
huo huo mkazi wa kijiji cha Lema tarafa ya Ntembela wilaya ya Kyelaaliyefahamika
kwa jina la Bicco Mwakibibi(28) aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili
wake kutoka kwa kutumia silaha za jadi za mawe na fimbo kutoka kwa wananchi
waliomtuhumu kwa vitendo vya wizi.
Kamanda
Msangi alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 12 majira ya saa 11 jioni
ambapo kundi la wananchi wenye mawe na fimbo waliamua kujichukulia sheria
mkononi baada ya kuwepo kwa madai kuwa marehemu alivunja kibanda cha biashara
na kuiba.
Alisema
hata hivyo marehemu alidaiwa kuwa alikuwa na mwenziye wakati wakitekeleza wizi
huo ambapo alikimbia baada ya tukio hilo huku akiendelea kutafutwa na Jeshi la
Polisi.
Post a Comment
Post a Comment