|
Baadhi ya askari polisi wakiwa katika eneo la ajali wakilinda usalama wa mali zilizokuwemo ndani ya Lori ambazo baadhi ya vibaka walikuwa wakitaka kujisevia |
|
Baadhi ya maboksi yaliyobeba sabuni yakiwa ndani ya Lori lililosababisha ajali maeneo ya Mbalizi. |
|
Mabaki ya Lori lililosababisha ajali katika eneo la Mlima Iwambi karibu na mji mdogo wa Mbalizi. |
|
Mabaki ya Lori |
|
Mkuu wa kituo cha Polisi jiji la Mbeya Richard Mchomvu akiwa sehemu ya ajali. |
|
Mabaki ya Basi aina ya Coaster ambalo liligongwa na Lori na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine 23 |
|
Mabaki ya Basi aina ya Coaster lenye namba za usajili T 910 BFB |
|
Hivi ndivyo ilivyokuwa ajali hiyo iliyohusisha Lori na Coaster katika eneo la Mbalizi |
|
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 10:45 leo jioni katika eneo la Mlima Iwambi kuelekea Mbalizi |
|
Baadhi ya askari polisi wakilinda mali zilizokuwemo katika Lori, hata hivyo askari hao walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya watu waliotaka kupora bidhaa hizo. |
|
Mmoja wa majeruhi wa ajali akiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya akisubiri kupatiwa matibabu. |
|
Wauguzi wa huduma ya haraka katika hospitali ya Rufaa Mbeya wakimpatia huduma mmoja wa
majeruhi wa ajali hiyo.(Picha kwa hisani ya Charles Abraham wa Malafyale Blog) |
WIMBI la ajali katika miezi ya
Disemba na Januari nchini limeendelea baada ya ajali nyingine kutokea mkoani
Mbeya leo jioni majira ya saa 10:45 katika
mtelemko wa Mbalizi na kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi
wengine 23.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio
hilo ni kwamba magari mawili moja aina ya Coaster na Lori la mizigo yalikuwa
yakielekea njia ya Tunduma kutokea Jijini Mbeya ambapo lori hilo linadaiwa
kuharibika mfumo wa breki likiwa mtelemkoni.
Lori hilo la mizigo aina ya SCANIA lenye
namba za usajili T 101 CRL na trela lenye namba za usajili T 859 BZW ambalo
lilibeba bidhaa mbalimbali za madukani liliigonga Coaster yenye namba za
usajili T 910 BFB na kusababisha magari hayo kupinduka.
Mashuhuda hao walidai kuwa wakati
Lori hilo likitelemka kwa kasi katika mlima huo mbele yake kulikuwa na gari
aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T 370 AST ambalo lilikuwa
likipandisha mlima na hivyo kumchanganya dereva ambaye alijikuta akiigonga
Coaster kwa nyuma.
Mmoja wa askari wa Usalama
barabarani aliyekuwepo eneo la tukio alidai kuwa wameshuhudia watu wawili
waliokufa papo hapo na abiria wengine 23 wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa
Mbeya na Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mbeya Barakael Masaki alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
kusema kuwa watu wawili ambao ni mwanamke na mwanaume mmoja ambao majina yao
hayajatambuliwa walifariki dunia katika ajali hiyo.
Aidha katika hali isiyo kuwa ya
kawaida askari wa kutuliza ghasi walilazimika waliofika katika eneo la ajali
walilazimika kufyatua risasi za moto hewani kwa nia ya kuwatawanya watu
waliofika katika eneo la ajali na kutaka kupora bidhaa zilizokuwemo ndani
ya lori.
Post a Comment
Post a Comment