Ads (728x90)

Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu tawala wapya wa mikoa mitano ambapo aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya Juma Rashid Idd ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Juma Idd ambaye uteuzi wake umechukua muda mrefu hata baadhi ya watu kudai kuwa huenda amepigwa majungu na baadhi ya wanasiasa wa Jiji la Mbeya ambapo nafasi yake ya Ukurugenzi ilichukuliwa na Mussa Zungiza aliyehamia kutokea Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ambako hakukaa muda mrefu akitokea Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Juma Idd aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha
Awali kabla ya Idd akiwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya kuliibuka tetesi za kuwepo kwa njama za kumng'oa ambapo baadhi ya wanasiasa walidaiwa  kusuka mkakati wa kumng'oa kwa kile kilichoelezwa kuwa msimamo wake ulikuwa unakitakia mabaya Chama Cha Mapinduzi CCM.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue iliyotolewa na Ikulu Jijini Dar es salaam alisema uteuzi na uhaamisho huo umeanzia jana Januari 18 ambapo aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sipora Liana anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI na nafasi yake inazibwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Rashid Idd.

Makatibu Tawala wapya walioteuliwa ni pamoja na Wamoja Dickolangwa ambaye anakuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa ambako alikuwa akikaimu nafasi hiyo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Newala Abdallah Chikota ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi na Symthies Pangisa ambaye alikuwa aliyekuwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara amekuwa Katibu Tawala mkoa wa Rukwa.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora Alfred Luanda sasa anakuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mtwara ilhali aliyekuwa Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Arusha Jackson Saitabahu sasa anakuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe.
 
Beatha Swai ahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI
Taarifa hiyo ya Ikulu imewataja  aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Pwani Beatha Swai sasa anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Benedict Kuyan aliyekuwa Katibu Tawala aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga anahamishiwa mkoa wa Mara na aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Rukwa Salum Chima anahamishiwa mkoa wa Rukwa.

Salum Mohamed Chima sasa Katibu Tawala mkoa wa Tanga

Mhandisi Omar Chambo ameteuliwa kuwa Katibu Tawala mkoa wa Manyara
Wengine waliohamishwa ni pamoja na Mgeni Baruani aliyekuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe sasa anahamishiwa mkoa wa Pwani, Mhandisi Omar Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi anakuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara na Dkt John Ndunguru aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi anakuwa Katibu Tawala mkoa wa Kigoma.

 


Post a Comment

Post a Comment