‘’Kila
kiongozi huja na mabadiliko yake ili kukamilisha ufanisi wake wa kazi, Malinzi
kaja na safu yake kwa mtazamo alionao, nimevunja mkataba na Timu ya Taifa, sijutii
uamuzi wake kwa kuwa ndivyo alivyoona inafaa, nimepokea kwa mikono miwili,mabadiliko
haya,’’Ndivyo alivyoeleza kocha Mdenish
Kim Poulsen aliyelazimika kuvunja mkataba wake wa kuifundisha timu ya Taifa
kutokana na mtazamo wa Rais wa sasa wa TFF Jamal Malinzi.
Aliyekuwa Kocha wa Stars Kim Poulsen |
Rais wa TFF Jamal Malinzi |
Rais Mstaafu wa TFF Leodgar Tenga |
Kutokana na
mtiririko wa mambo mengi yaliyojiri kabla ya uteuzi katika mchakato wa kuwania
kiti cha Urais wa chama Cha Mpira wa Miguu nchini TFF yapo mengi ya kujifunza
juu ya mustalabali wa soka la Tanzania na aina ya viongozi wanaokalia kiti
hicho.
Malinzi
anakuwa ni Rais wa Pili tangu kuanzishwa kwa Shirikisho la Soka nchini TFF
baada ya kile kilichokuwa chama cha Mpira wa miguu nchini FAT.
Matumaini ya
soka la Tanzania hutegemea zaidi mtazamo wa kiongozi aliye madarakani ingawa
kiongozi huyo hafanyi kazi kama yeye bali hufanya kwa niaba ya taasisi nzima,
bali uamuzi wa juu wa kiongozi ndio unaoonekana kuheshimiwa zaidi.
Inawezekana kwa
kujua kuwa uamuzi unaotolewa hutokana na maamuzi ya jopo la viongozi wa TFF
ndio hasa imekuwa sababu ya kubadilisha safu ya uongozi wa juu ili
kumrahisishia utendaji Rais Malinzi katika maamuzi yake.
Sipendi
kusema mengi yaliyosemwa hapo awali juu ya ‘Interest’ iliyooneshwa na kiongozi
huyu hadi ikatafsiriwa kuwepo kwa ubaguzi na hata kueleza kuwa kuna ukabila
unaingizwa katika soka la Tanzania, bali kinachoendelea kutendeka kinaonesha
dira ya kutumbukia mtaroni kwa soka letu.
Ipo hoja
miongoni mwa wadau wa soka wakielezea mtazamo wao juu ya Malinzi kama kweli ana
uchungu na soka la nchi yetu ama anachokifanya ni njia ya kujijengea hadhi na
heshima binafsi kutokana na maamuzi anayoyafanya ndani ta soka la nchi yetu.
Tunaweza
kusema Malinzi ana uchungu sana na soka
la nchi yetu hata kuamua kukatisha mkataba wa Kim Poulsen nyuma ya miezi minane
na hata kulazimika kutoa fedha zake za
mfukoni, ingawa si muhimu kujua atazirudishaje fedha hizo mfukoni mwake kwa
kipindi cha uongozi wake, ‘’hapa tuiachie TAKUKURU ifanye kazi yake’’.
Ninavyokumbuka
Poulsen aliingia nchini akitokea Denmark mwaka 2010 akifundisha vijana wa chini
ya miaka 17 Serengeti Boys na wale wa chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes na baadaye kuwa kocha wa timu ya Taifa akirithi
mikoba ya mtangulizi wake Mdenish mwenzie Jan Poulsen.
Poulsen
amedumu katika Timu ya Taifa tangu Mei 14 2012 na kukamilisha safari ya siku 645
tangu aanze kuifundisha Stars akizidiwa na mtangulizi wake Jan aliyedumu na
Stars kwa takribani siku 730 ambapo baadaye hakuongezewa mkataba mwingine na
TFF kuendelea kuifundisha Stars.
Tutaendelea
kubanwa na historia ya soka la nchi yetu kufundishwa na makocha wakigeni huku
kila kocha aliyepata kuifundisha timu ya Taifa akiondoka na historia ya aina
yake kutokana na mtazamo wa viongozi waliopo madarakani.
Yapo mengi
ya kujiuliza juu ya mabadiliko anayoyafanya Malinzi kuanzia pale alipoamua
kupangua safu ya viongozi wa juu wa TFF ambapo kwa hatua hiyo hoja nyingi zinaibuliwa
kwa kile kilichoelezwa kuwa anaendeleza ukabila ijapo alikanusha taarifa hizo
kuwa yeye anafuata watendaji bora hafuati kabila la mtu.
Ijapokuwa ni
mapema kuelezea mustakabali wa soka la nchi yetu kwa siku 100 za Malinzi bali
ni muhimu kuweka angalizo kwa namna ambavyo ameanza kwa kasi ya kujenga chuki
kwa watendaji waliomtangulia katika uongozi wake…!!
‘’Wacha
Niseme Ya Moyoni Mwangu juu ya Mtazamo Wangu Na Mustakabali wa Soka Letu Nchini’’Alamsiki!!!
Post a Comment
Post a Comment