LIGI kuu ya
Vodacom imeendelea leo jioni katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya kwa
kuzikutanisha timu za Mbeya City na JKT Oljoro ambapo hadikipyenga cha mwisho
kinapulizwa timu hizo zimetoka suluhu ya bila kufungana.
Mechi hiyo
ambayo ilihudhuriwa na watazamaji wachache kutokana na tiketi kuuzwa sh.5,000
badala y ash. 3,000 ilianza kwa kasi kwa kila timu kulishambulia lango la
mwenzie.
Mashabiki
wachache waliohudhuria mechi hiyo walikosa ladha halisi ya mchezo huo kutokana
na timu hizo kutoonesha kandanda safi na hivyo kuwa ni mpira wa piga nikupige.
Hadi
Kipindi cha kwanza kinamalizika timu
zote zitoka uwanjani bila kufungana ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kila
timu kufanya mabadiliko, Mbeya City walibadilisha wachezaji wa watatu na JKT
Oljoro ilibadilisha wachezaji wawili.
Mbeya City
iliwaingiza Peter Mapunda badala ya Francis Casto,Mwagane Yeya aliingia badala
ya Jeremiah John na Deus Kaseke aliingia badala ya Alex Sethi, wakati kwa
upande wa timu ya Oljoro Hasira Hamis aliingia badala ya Uda Solita na Paul
Malipesa alichukua nafasi ya Babu Ally Seif.
Hadi kipenga
cha kumaliza mpira cha mwamuzi Martin Saanya kinapulizwa timu hizo zimetoka
suluhu ya bila kufungana.
Katika hatua
nyingine Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Mbeya (MREFA) aliwaomba
radhi wapenzi wa soka Jijini Mbeya kutokana na tiketi kuuzwa bei ya Sh.5,000
badala ya Sh.3,000 na bei hiyo imepangwa na Shirikisho la Soka nchini TFF.
Alisema hali
hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza mapato ya mechi hiyo kutokana na
idadi ya mashabiki wachache walioingia uwanjani ikiwa ni pamoja na tiketi
kuchelewa kuuzwa.
Leoligi hiyo
inaendelea kwa kuwakutanisha maafande wawili ambao ni timu mwenyeji ya Prison
inayoikaribisha timu ya Mgambo JKT kutoka mjini Tanga.
Post a Comment
Post a Comment