Kikundi cha sanaa cha nyimbo za Asili cha Wane Star kilitoa burudani kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013 |
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga akisoma hotuba kabla ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013 |
Baadhi ya wanahabari wakiwa na Tuzo na zawadi Umahiri wa Uandishi wa Habari wakishangilia ushindi mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. |
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari nchini (MCT) Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa wanahabari 76 walioshiriki katika tuzo ya umahiri wa uandishi bora nchini. |
Baadhi ya wanahabari wakishiriki katika hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari bora nchini. |
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Joseph Kulangwa akishangilia jambo wakati wa utoaji wa tuzo za Umahiri wa Uandishi Bora nchini |
Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Joseph Kulangwa akimpongeza mwandishi wa habari wa gazeti hilo Khadija Mussa aliyeshinda tuzo ya habari za uandishi wa Utawala Bora |
Jaji Mstaafu obert Kisanga akijadili jambo na Rais wa Majaji wa Afrika Mashariki Harold Nsekela huku wakishuhudia waandishi mahiri wakipita jukwaani na kupokea tuzo na zwadi zao |
Wageni kutoka ndani na nje ya nchi walialikwa katika hafla hiyo mahususi kwa wanahabari waliofanya vizuri zaidi katika kazi za habari mwaka 2013 |
Waandishi walipata fursa ya kuchat huku wakibadilishana mawazo wakisubiri kupata tuzo na zawadi walizoandaliwa na Baraza la Habari nchini (MCT) |
Dkt. Mengi akifurahia burudani iliyokuwa ikirendelea katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013 |
Mwandishi wa habari mwandamizi Abdallah Majura akifurahia a tuzo yake ya habari za Uchunguzi kwa vyombo vya Redio huku Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari Dkt. Mengi akifurahia. |
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga akitoa hotuba kabla ya ugawaji wa Tuzo na Zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013 |
Mwandishi wa habari mwenye mafanikio ya maisha katika habari Mariam Hamdan akipongezwa |
Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One Joyce Mhavile akisoma wasifu wa mwandishi mahiri mwenye mafanikio katika kazi za Uandishi wa Habari Mariam Hamdan |
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari MOAT Dkt. Reginald Mengi akimkabidhi luninga Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Uandishi wa Habari nchini Idd Juma kutoka Afya Redio ya Jijini Mwanza. |
Mchora katuni bora wa mwaka 2013 Muhidin Msamba akiwa na tuzo yake mara baada ya kutangazwa kuwa ni mchora katuni bora nchini |
Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One Asraji Mvungi akipokea tuzo za uandishi wa habari bora za Watoto kupitia Luninga |
Msanii mahiri wa nyimbo za asili Wane Star akitoa burudani wakati hafala ya utoaji wa utoaji wa zawadi na tuzo kwa wanahabari mahiri nchini. |
Post a Comment
Post a Comment