Ads (728x90)

KWA NIABA YANGU NA FAMILIA YANGU, NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU NA WAZAZI WANGU WALIONILETA DUNIANI NA KUNILEA AMBAO KWA SASA BAADHI YAO WAKO MBELE YA HAKI KWA KUNIJAALIA KUKARIBIA KUFIKISHA NUSU KARNE,NAAMINI WANGEKUWEPO WOTE LEO HII, NINGEJIFANYA MTOTO NA KUKETI KARIBU NAO, NINGEWAITA KWA MAJINA YAO ADHIIMU TULIYOZOEA KUWAITA, BABAA!!! MAMAAA!! NA WANANGU WANGEWAITA!! BABUUU!!! BIBII!!! LAKINI BAHATI MBAYA NIMEKOSA FURSA HIYO,NITAJITAHIDI KUWAENZI JAMAA NA MARAFIKI WA WAZAZI WANGU NAAMINI KWA KUFANYA HIVYO THAWABU ITAWAFIKIA WALIKO MBELE YA HAKI,HATA HIVYO BADO NAMTHAMINI MAMA YANGU ALIYOKO SASA NAMPENDA NA KUMJALI KWA KUWA ANANIPENDA NA KUNIJALI, AMENILEA NA KUNIKUZA HADI NIMEFIKIA UMRI HUU, SINA LA KUMLIPA, BADO NAKUTHAMINI MAMA YANGU, MUNGU ATAKUPUNGUZIA MARADHI YA UTU UZIMA, NAAMINI ANGEKUWEPO BABA YANGU LEO HII UNGEKUWA KAMA BADO NI KIJANA, NAWASHUKURU NDUGU NA JAMAA ZANGU NINAOISHI NAO KWA SASA HUKU UGHAIBUNI, MBALI NA NILIKOZALIWA,MBALI NA CHANGAMOTO LUKUKI NINAZOKUTANA NAZO KATIKA JAMII NIISHIYO, BADO TUNASAMEHEANA NA MAISHA YANASONGA MBELE, NAWAOMBA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI ZANGU MUENDELEE KUNISAMEHE KW AMAKOSA NIYAFANYAYO AMBAYO NI YA KIBINADAMU, MAANA HAKUNA BINADAMU MKAMILIFU, NAMI NACHUKUA FURSA HII KUWASAMEHE WALIONIFANYIA INDA, KWANI NAAMINI ALIYEKAMILIKA NI MWENYEZI MUNGU PEKEE, NI VIGUMU KUWATAJA MMOJA MMOJA KATIKA ORODHA NDEEFU YA MARAFIKI ZANGU, BALI KWA UMUHIMU WA KIPEKEE,NAWASHUKURU BLOGERS WOTE WA NDANI NA NJE YA NCHI,WANAHABARI WOTE WA NDANI NA NJE YA NCHI AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE TUMEKUWA TUKIBADILISHANA MAWAZO KUPITIA KALAMU ZETU, AIDHA NAISHUKURU KAMPUNI YA UCHAPISHAJI MAGAZETI YA BUSINESS TIMES, INAYOTOA MAGAZETI YA MAJIRA,BUSINESS TIMES,SPOTI STAREHE NA MAISHA, PIA REDIO TIMES FM YA JIJINI DAR AMBAO WOTE KWA PAMOJA WAMENIPA NGUVU YA KUKUTANA NA JAMII ILIYOMBALI AMBAO WAMEKUWA WAKIZISOMA NA KUZISIKIA KAZI ZANGU KUPITIA VYOMBO HIVYO, NAWASHUKURU PIA WASOMAJI WA MAKALA NA KAZI ZANGU AMBAO WAMEKUWA WAKINISAPOTI KWA KUNIPIGIA SIMU BAADA YA KUZISOMA KAZI ZANGU, PIA NAWASHUKURU WADAU WENGINE KAMA VILE TAMWA,TMF,HAKI ELIMU,TGNP,MISA-TAN,GEMSA,MCT,UTPC NAWENGINE AMBAO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE WAMEKUWA WAKIZIJALI KAZI ZANGU NA KUZIFANYIA KAZI, PIA KWA UPEKEE NAWASHUKURU WAHARIRI MBALIMBALI NILIOWAHI KUFANYA NAO KAZI, MAGAZETINI, WANAHABARI WA MKOA WA MBEYA, CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MBEYA, AMBAO KUTOKANA NA MSUKUMO HUO NIMEFANIKIWA KUWA MIONGONI MWA WANAHABARI 76 WENYE KAZI 101 AMBAZO ZINAWANIA TUZO YA EJAT, ITAKAYOFANYIKA KESHOKUTWA JIJINI DAR, NAAMINI HII NI FURSA PEKEE YA KUADHIMISHA UMRI NILIOUFIKIA KWA FURAHA, RAHA NA FARAJA, KWANI MIE SINA UJANJA WA KUNIWEZESHA KUFIKISHA UMRI HUO, NI MUNGU PEKEE, KANICHANGUA MIONGONI MWA WENGI WALIOTANGULIA MBELE YA HAKI ILI NIBAKI NISHUHUDIE MALIMWENGU YANAYOTOKEA, SINA LA KUSEMA ZAIDI YA KUMSHUKURU KWA KUSEMA ALHAMDULILLAHI!!!

Post a Comment

Post a Comment