WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais(Utawala Bora) George Mkuchika amewataka watumishi wa umma kuzingatia maadili katika utendaji wao ili kuepuka watendaji kupigiwa mifano ya utoaji na upokeaji Rushwa.
Mkuchika alisema hayo katika Mkutano wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya(RCC) katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa na kusema kuwa kila kiongozi akizingatia maadili ni dhahiri mienendo mibaya inayohusishwa na vitendo vya rushwa itadhibitiwa.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya nne inaamini ujenzi na uimarishaji wa Utawala Bora ndiyo njia pekee yenye ubora sahihi na yenye uhakika katika jitihada za kuondokana na matatizo ya rushwa, umaskini na uendeshaji mbovu wa huduma za umma.
Alisema serikali kwa kuzingatia muongozo wa Taaifa wa mwaka 1999 kuhusu Utawala Bora(Good Governance) imeanzisha programu mbalimbali kwa lengo la kujenga na kuimarisha Utawala Bora nchini.
Mkuchika alisema kuwa baadhi ya programu hizo ni marekebisho ya kuboresha utendaji katika utumishi wa umma(The Public Service Reform Programe) na marekebisho ya kuboresha usimamizi wa fedha za umma (The Public Financial Management Programme) na mareekebisho ya kuboresha mfumo wa uendeshaji wa serikali za mitaa( The Local Government Reform Programme).
Alisema programu nyingine ni marekebisho katika sekta ya sheria, mkakati wa kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini-MKUKUTA na Mkakati wa Kitaifa Dhidi ya Rushwa na mpango wa Utekelezaji.
Post a Comment
Post a Comment