MKUTANO WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS CONFERENCE” TAREHE 18.04.2014.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatumia fursa hii
kukutana na Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya kutoka Vyombo mbalimbali vya
Habari ikiwa ni nafasi ya kutoa tathmini ya Hali ya Uhalifu kwa Mkoa wa Mbeya kwa
kipindi cha robo – mwaka Jan-Machi, 2014, pia kusikia maoni, ushauri na
changamoto mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari kwa lengo la kujenga na
kuboresha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA JAN-
MACHI, 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- MACHI, 2013.
MACHI, 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- MACHI, 2013.
1. TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya
makosa 6,473 yaliripotiwa, wakati
kipindi kama hicho mwezi Jan – Machi, 2013
makosa 6,853 yaliripotiwa, hivyo
kuna pungufu ya makosa 380 sawa na asilimia 6.
2. TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Jan – Machi, 2014 jumla ya
makosa makubwa 594 yaliripotiwa,
wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013
makosa 601 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 7 sawa na asilimia 1.
3. TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA
ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.
Aidha
katika kipindi cha Jan – Machi, 2014 makosa makubwa yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali
katika kufanya doria,misako na operesheni katika kupambana na uhalifu na
wahalifu yaliripotiwa matukio 128, wakati
kipindi cha Jan- Machi, 2013 yaliripotiwa makosa 121, hivyo kuna ongezeko la matukio 7, sawa na asilimia 84
4. TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
§ Kwa
upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yote
yaliyoripotiwa katika kipindi cha Jan – Machi,
2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na
usafirishaji ni 12,250 wakati
kipindi kama hicho Jan-Machi, 2013
yaliripotiwa makosa 14,375 hivyo
kuna pungufu ya makosa 2,125 sawa na asilimia 15.
§ Matukio
ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Jan
– Machi, 2014 yalikuwa 98 wakati
kipindi cha Jan- Machi, 2013 yalikuwa
156 hivyo kuna upungufu wa matukio 58 sawa
na asilimia 37. Matukio ya ajali za vifo
yaliyoripotiwa Jan – Machi, 2014
yalikuwa 58 wakati kipindi cha Jan-Machi, 2013 yaliripotiwa matukio 65 hivyo kuna pungufu ya matukio 7 sawa na asilimia 11.
§ Watu
waliokufa kipindi cha Jan-Machi, 2014
walikuwa 61 wakati Jan –Machi, 2013 walikuwa 81 hivyo kuna pungufu ya watu 20, sawa
na asilimia 7. Watu waliojeruhiwa
kipindi cha Jan – Machi, 2014 walikuwa
watu 104 wakati Jan – Machi, 2013 walikuwa watu 91 hivyo kuna ongezeko la
watu 13, sawa na asilimia 14.
§ Katika
kipindi cha Jan – Machi, 2014, jumla ya makosa 12,422 ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani
na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 332,790,000/= ikilinganishwa na tozo la Tshs 365,400,000/= iliyokusanywa
katika kipindi Jan – Machi, 2013 kutokana na makosa 14,219, hivyo kuna pungufu
la kiasi cha Tshs 32,610,000/= sawa na asilimia 9.
5.
MAJEDWALI KUONYESHA HALI YA UHALIFU.
MCHANGANUO WA MAKOSA
YOTE MAKUBWA YA JINAI NA USALAMA
BARABARANI KWA KIPINDI CHA FEB - 2014
IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN - MACHI, 2013.
MAKOSA
|
JAN–
MACHI 2014
|
JAN
– MACHI 2013
|
TOFAUTI +/-
|
ASILIMIA %
|
MAKOSA DHIDI YA BINADAMU
|
||||
MAUAJI
|
53
|
82
|
-29
|
-35
|
KUBAKA
|
129
|
98
|
+31
|
+32
|
KULAWITI
|
14
|
5
|
+9
|
+180
|
KUTUPA MTOTO
|
2
|
5
|
-3
|
-60
|
USAFIRISHAJI BINADAMU
|
3
|
1
|
+2
|
+200
|
JUMLA
|
201
|
191
|
+5
|
+3
|
-
Mauaji - Wilaya iliyoongoza ni Mbeya
13,Momba 10 na Chunya 9.
-
Kubaka- Wilaya iliyoongoza ni Mbeya
60, Chunya 21 na Rungwe 14.
-
Kulawiti – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 6 na Mbarali 2.
-
Usafirishaji wa binadamu – Wilaya iliyoongoza ni Mbozi 1/Momba 1 na Mbarali 1.
MAKOSA DHIDI YA KUWANIA MALI
|
||||
UNYANG’ANYI WA K/SILAHA
|
3
|
4
|
-1
|
-25
|
UNYANG’ANYI WA K/NGUVU
|
25
|
46
|
-21
|
-46
|
UVUNJAJI
|
92
|
109
|
-17
|
-16
|
WIZI
|
873
|
989
|
-116
|
-12
|
WIZI WA PIKIPIKI
|
52
|
26
|
+26
|
+100
|
WIZI WA MIFUGO
|
59
|
59
|
-
|
-
|
JUMLA
|
1,104
|
1,233
|
-129
|
-10
|
-
Unyang’anyi ktk Barabara Kuu – Wilaya iliyoongoza ni Mbarali 1.
-
Unyang’anyi wa kutumia nguvu – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 8 na Momba 8/Chunya 8.
-
Uvunjaji - Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 22, Momba 18 na Kyela 13.
-
Wizi wa Pikipiki –Wilaya iliyoongoza ni Chunya 18, Mbeya 14 na Kyela 8
-
Wizi wa Mifugo – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 10, Mbarali 3 na Chunya 2.
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
[YATOKANAYO NA JITIHADA ZA POLISI KWA USHIRIKIANO NA WADAU NA WANANCHI
MBALIMBALI]
|
||||
KUPATIKANA NA SILAHA
|
8
|
4
|
+4
|
+100
|
BHANGI
|
60
|
66
|
-6
|
-9
|
NYARA ZA SERIKALI
|
4
|
-
|
-4
|
+400
|
POMBE YA MOSHI.
|
48
|
24
|
+24
|
+100
|
WAHAMIAJI HARAMU
|
3
|
19
|
-16
|
-84
|
JUMLA
|
123
|
113
|
+10
|
+9
|
-
Kupatikana na silaha - Wilaya iliyoongoza ni Chunya
3 na Mbozi 2 .[Silaha aina ya
Gobole 6, Riffle 1 na Bastola ya
kienyeji 1]
-
Kupatikana na bhangi –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 21,
Rungwe
7 na Chunya 7. [Uzito
wa Kilo 94 na Gram 734 pamoja na shamba moja la bhangi yenye ukubwa warobo hakari ¼ na miche 314 ]
-
Kupatikana na pombe ya moshi[gongo] – Wilaya iliyoongoza ni Chunya 15, Mbeya 14 na Mbarali 4.[Ujazo wa lita 99 na mitambo 6]
-
Wahamiaji haramu –Wilaya iliyoongoza ni Mbozi 1/Momba 1na Mbarali 1.
[Wahamiajai
haramu 28 - Somalia 4,Pakistan 7 na Ethiopia 17]
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI
CHA JAN-MACHI, 2014 NA JAN – MACHI, 2013.
|
||||
MATUKIO
|
12,250
|
14,375
|
-2,125
|
-15
|
MATUKIO YA AJALI
|
98
|
156
|
-58
|
-37
|
AJALI ZA VIFO
|
58
|
65
|
-7
|
-11
|
WALIOKUFA
|
61
|
81
|
-20
|
-7
|
WALIOJERUHIWA.
|
104
|
91
|
+13
|
+14
|
AJALI ZA MAJERUHI
|
40
|
91
|
-51
|
-56
|
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
|
12,422
|
14,219
|
-1,797
|
-13
|
TOZO [NOTIFICATION]
|
332,790,000/=
|
365,400,000/=
|
-32,610,000/=
|
-9
|
-
Matukio yote yaliyoripotiwa –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 7,051, Mbarali 1,633 na Momba
1,142.
-
Matukio ya
ajali – Wilaya
iliyoongoza ni Mbeya 51, Rungwe 14 na Mbarali
7.
-
Ajali za Vifo – Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 20, Rungwe 14 na Mbarali 7.
-
Watu waliokufa –Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 22, Rungwe 17 na Mbarali
7.
-
Watu waliojeruhiwa - Wilaya iliyoongoza ni Mbeya 65, Rungwe 13 na Kyela 9.
WITO WA KAMANDA:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi Ahmed Z. Msangi anatoa
wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Jeshi la Polisi
kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati za wahalifu na uhalifu katika maeneo
mbalimbali pale waonapo viashiria ambavyo si vya kawaida au pindi tukio
linapojitokeza ikiwa ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno, mazungumzo ya simu
au kwa kufika moja kwa moja kituo cha Polisi Kilipo Karibu na maeneo yao.
Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawahakikishia
Wananchi/Wakazi wa Mkoa wa Mbeya na Wageni wote hali ya Amani na Utulivu katika
Kipindi hiki cha kusherehekea Sikukuu ya Pasaka. Kila Mwananchi aone anawajibu
wa kufuata na kutii sheria zilizowekwa bila kushurutishwa. Pia rai kwa wananchi
kuacha muangalizi/waangalizi nyumbani wanapotoka kwenda katika Ibada za Mkesha
na Sherehe kwa jumla kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mali zao.
Kwa watumiaji wa Vyombo vya Moto wafuate na kuzingatia
Sheria na Alama za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali. Halikadhalika watembea
kwa miguu kuwa makini na matumizi ya barabara ikiwa ni pamoja na kuvuka katika
maeneo yenye vivuko [zebra crossing].
Aidha Kamanda wa Polisi anawataka wazazi/walezi kuwa
makini na watoto wadogo kwa kutowaacha wakatembea bila uangalizi wa kutosha.
Wamiliki wa kumbi za Starehe kuzingatia taratibu za uendeshaji wa Biashara zao
ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya pia anatoa shukrani
kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha
kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi kwa njia ya kuhabarisha umma.
Nitumie nafasi hii kuwatakia Sikukuu njema ya Pasaka,
kwa kuungana na Wakristu Dunia kote kusherehekea kufufuka kwa Yesu Kristo.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment