Waziri Mkuu Mizengo Pinda |
Hawa Ghasia Waziri TAMISEMI |
Na Kibada Kibada, Mlele
Halmashauri ya Nsimbo
wilayani mlele mkoani katavi imefanikiwa kukusanyajumla ya shilingi milioni
753.04 na kuvuka lengo kwa asilimia 5.6 ya lengo lililowekwa la kukusanya jumla
ya shilingi milioni 713,328.000.kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Hayo yamelezwa na
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Rashid Neneka wakati akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 kwenye kikao cha mkutano
mkuu wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Neneka ameeleza kuwa
katika kikao maalum cha madiwani cha kupitisha bajeti kwa halmashauri hiyo
ilipitisha kiasi cha shilingi bilioni 17,596,313,000 kutoka vyanzo mbalimbali
vya mapato.
baada ya kupata ukomo wa
bajeti kutoka hazinaTAMISEMI makisio ya bajeti yamepungua kwa asilimia 22
hadi kufikia shilingi bilioni 13,682,949,500 kutoka vyanzo mbalmbali vya
mapato
Neneka amevitaja vyanzo
hivyo kuwa mapato ya ndani fidia ya vyanzo vilivyofutwa, miradi ya
maendeleo.fedha za ndani fedha za wafadhili pamoja na vyanzo vingine.
Akizungumzia miradi ya
maendeleo ameelezakatika kipindi cha robo ya pili yatu na yanne katika mwaka wa
fedha wa 2013/2014 idara ya mipango imepeleka kiasi cha fedha milioni 342 kwa
ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kati ya fedha hizo milioni 282 zilielekezwa
kwa sekta ya Elimu ya Msingi na shilingi milioni 60 zilielekezwa kwenye ujenzi
sekta ya Elimu ya Sekondari.
Aidha ameeleza kuwa
idara ya mipango ilisimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo madiwani
walipita kuikagua katika ziara zao za kuhimiza Miradi ya maendeleo yenye
thamani ya shilingi bilioni 1.2 .
Miradi hiyo iko katika
sekta ya Elimu, Afya,Maji,Utawala ,Barabara na Umwagiliaji,miradi ambayo
imetekelezwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa maaendeleo 2013/2014.
Post a Comment
Post a Comment