Akina baba nao hawakuwa nyuma katika michezo nao walishiriki kwenye mchezo wa kuvuta kamba ili kupimana nguvu baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan |
Waislamu pia walijitokeza katika mashindano ya mbio za baiskeli ili kukamilisha burudani ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Jijini Mbeya. |
Baadhi ya akina mama wa Kiislamu wakijiandaa kwa mchezo wakati wa Tamasha la Eid El Fitri katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya jana alasiri. |
Mbali na michezo mingine iliyofanyika, kulikuwa na mchezo mwingine wa kuvutia wa mashindano ya Kukuna Nazi kwa akina baba na akina mama |
Aidha Tamasha hilo la Eid El fitri lilihitimishwa kwa mechi ya burudani kati ya Maimamu na timu ya Mbeya City kikosi cha pili ambapo Mbeya City waliibuka na ushindi wa mabao 3-1. |
Benchi la Ufundi la timu ya Maimamu |
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakifuatilia michezo mbalimbali ya Tamasha la Eid El Fitri kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine |
Wachezaji wa Mbeya City wakipata mawaidha baada ya kumalizika kwa mechi kati yao na timu ya Maimamu |
Awali wakati wa adhuhuri baadhi ya waumini wa dini hiyo walipata fursa ya kualikwa kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa mmoja wa waumini hao Amour Sumry |
Walikula chakula na vinywaji na kushiba kabla ya kuingia kwenye tamasha la Eid |
Vyakula aina mbalimbali viligaiwa kwa Mashekhe ambao walikula na hatimaye kusaza!!! nadhani hii ilitokana na matumbo yao kutozoea kula mchana kwa takribani mwezi mzima wa funga ya Ramadhan |
Post a Comment
Post a Comment