Bango Kubwa la kalenda la mmoja wa viongozi wa serikali ni kati ya mabango mengi yaliyoibuka katika maeneo mbalimbali yanayoashiria nia ya kuwania Uongozi wa juu wa nchi mwaka 2015 |
Tunahesabu takribani miezi 15 kufikia Octoba mwaka 2015, kwa siku hizo ambazo zimekuwa zikipeperuka kama upepo baadhi ya wanasiasa hususani wale walioko ndani ya chama tawala wamekuwa wakijwekea mazingira ili kufika Ikulu kwa njia tofauti tofauti.
Wapo wanaojiweka hadharani na wakuu wao kuwabeza kwamba bado hawajatosha kufikia hatua hiyo, bali pia wapo wanaotumia njia za Kiielekroniki kwa kutumia mitandao ya Kijamii, FaceBook, Twitter Instagram, Whatsup na hata wengine wamefungia Blogu na vyombo vya habari kwa nia ile ile ya kujiwekea njia rahisi ya kupenya kufika Ikulu.
Aidha wengine wanatumia vipeperushi huku wakiwapa dili wamiliki wa Stationaries kwa kutengeneza mabango makubwa, tisheti na hata kalenda, ilimradi kila mmoja akitaradhia kuifikia miezi hiyo 15 kwa fanaka na tija ni kama vile kuna ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba lazima watafikia huko.
Post a Comment
Post a Comment