Na Kibada Kibada -Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe amewataka vijana
kote mkoani Katavi kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo ili
kujikomboa kuondokana na umasikini kwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia fursa
zilizopo mkoani humo.
Dkt Rutengwe ametoa rai hiyo wakati akikabidhi msaada wa
Mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa
Mkoani Katavi kwa vikundi vya Vijana waliojiunga Pamoja kuanzisha miradi ya
maendeleo itakayowaondolea umasikini.
Mbali ya kutoa wito kwa vijana kutumia fursa hizo pia
amewaasa wazazi wote mkoani huo kuzingatia elimu kwa vijana wao kwa kuwa elimu
pekee ndiyo itakuwa mkombozi wa maisha ya mwanadamu bila elimu hakuna
maendeleo.
Akawahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule ili waweze kupata
elimu na wale ambao hawakupata nafasi ya
kuendelea na elimu ya sekondari wawapeleke kwenye vyuo vya ufundi stadi Veta
wapate elimu ya ufundi ambayo itawasidia katika maisha ,kwa kuwa watakuwa na
ujuzi utakao wawezesha kujitegemea kwa kufanya kazi mbalimbali katika jamii
kama ufundi wa ujenzi na ufundi mwingine
Amewaasa vijana watumie nafasi hiyo waliyopata ya kupewa
misaada ya mashine za kufyatua tofali ili iwe chachu ya maendeleo kwao na kiw
kichocheo kwao kujileta maendeleo na vijana wengine waige kutoka kwao.
Awali Meneja wa SHIRIKA LA nyumba Mkoani Katavi na Rukwa
Nehemia Msigwa alieleza kuwa Shirika la nyumba Mkoani Katavi limetoa misaada ya
mashine za kufyatulia Tofali kwa vikundi vya vijana kwa Halmashauri nne za Mkoa
wa Katavi ili ziweze kuwasaidia vijana kujikwamua na umasikini kwa kuanzisha
miradi ya ufyatuaji tofali.
Msigwa alieleza kuwa
shirika lake limeamua kutoa msaada huo ili kuwasaidia Vijana kujianzishaia
miradi yao ili waweze kujiali kupitia kwenye miradi ya ufyatua tofali kwa
kutumia mashine hizo ambazo ni imara na bora na matoafali yanayotokana mashine
hizo ni bora na imara hivyo wataweza kuondokana na umasikini .
Msigwa ameleza kuwa shirika
la nyumba limebuni mpango wa kuwasaidia vijana kujiajili kwa kutumia mpango wa kuwasaidia vijana
mashine ya kufyatu matofali ili kuwaondolea
umasikini na limetoa mashine nne kwa kila Halmashauri za wilaya ziweze
kuwasaidia vijana kuondokana na umasikini na Halmashauri kupitia Idara za
Maendeleo ya Jamii Kitengo cha Vijana watasimamie miradi hiyo.
Amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Mpanda Mji ambayo imekabidhiwa
mashine nne na mbili wamenunue wenyewe kuwasaidia Vijana ,Halmashauri ya
Mpanda, Halmashauri ya Mlele na Nsimbo
Mbali ya kutoa msaada wa mashine za kufyatua tofali kwa
makundi ya vijana hao walijiunga pamoja katika vikundi vya uzalishaji mali ili
kuondokana na umasikini pia Shirika hilo limetoa fursa kwa vijana wenye
utalaamu katika fani ya uselemara mkoani humo kujitokeza kufanya kazi kwenye
shirika hilo mkoani humo ili waweze kujipatia kipato na kuondokana na
umasikini.
Fursa iliyotolewa ni kwa vijana 20 wenye fani hizo na
wengine kumi wenye fani ya ujenzi kufanya kazi katika shirika hilo mkoani hapo
kwa watoto walimaliza elimu ya ufundi kupitia kwenye chuo cha ufundi stadi Veta
Mpanda waweze kuaidia katika shughuli za ujenzi unaoendelea sehemu mbalimbali
Mkoani humo.
Meneja huyo wa shirika la nyumba ametoa fursa hiyo kufuatia
kuwepo kwa vijana wengi mitaani wakilalamika kuwa hakuna ajira wakati ajira
zipo lakini hawazitumie Vijana hao kwa kile wanachodhani ajira ni maofisini
tushirika la nyumba limekuja kuwawezesha vijana kujikomboa kuondokana na
umasikini Mkoani humo.
Post a Comment
Post a Comment