Mkuu wa Wilaya ya Momba Abihudi Saideya akiandika namba ya usajili katika mtumbwi wa uvuvi wakati wa uzinduzi wa Ziwa Rukwa ambalo lilifungwa kwa miezi 6 kutokana na uharibifu wa mazingira. |
Uoto wa asili umerejea baada ya Ziwa kufungwa kwa miezi 6 |
Wavuvi wakikokota Mtumbwi kuelekea Ziwani baada ya kusajiliwa kwa matumizi halali ya uvuvi ziwani humo |
ZANA za uvuvi
haramu zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 69 zimenaswa na kutekekezwa kwa
kipindi cha miezi sita cha kufungwa kwa Ziwa Rukwa wakati wa operesheni maalumu
iliyokuwa ikifanywa kuzuiwa wavuvi haramu Wilayani Momba Mkoani Mbeya.
Ziwa Rukwa
lilifungwa kwa miezi sita kutokana na tangazo maalumu lililohusisisha wilaya jirani
za Chunya mkoani Mbeya na Mlele wilayani Sumbawanga ambapo zilikubaliana kwa
pamoja kulinusuru ziwa hilo lililokumbwa na uharibifu wa mazingira, uvuvi
haramu na kusababisha kupungua kwa samaki ziwani humo.
Katika taarifa
iliyosomwa wakati wa kufunguliwa kwa Ziwa hilo kwenye kilele cha Siku za
Serikali za Mitaa kilichofanyika kijiji cha Samang’ombe ufukweni mwa ziwa hilo,
Ofisa Uvuvi Ali Libenanga alisema kuwa kwa kipindi cha miezi sita ya kufungwa
kwa ziwa hilo doria mbalimbali zilifanyika na kufanikiwa kukamata wavuvi haramu
wenye zana za uvuvi zenye thamani ya sh. Milioni 69.9.
Libengana ambaye
alisoma taarifa hiyo mbele ya Mkuu wa wilaya ya Momba Abihudi Saideya kwa niaba
ya Mkurugenzi wa Halmashauri Antony Mwantona alisema kuwa kwa kipindi cha kati
ya Januari na Mei katika forodha tofauti za wilayani humo zilikamatwa nyavu na
baruti zilizohusisha uvuvi haramu.
Alisema nyavu
hizo ziliteketezwa Machi 5 ambapo jitihada
za kuendelea kuhifadhi ziwa hilo zilitekelezwa kwa kuwahusisha wananchi wa
maeneo hayo kwa kuweka mikutano ya hadhara kwa nia ya kulitunza Ziwa hilo
pamoja na fukwe zake.
Miongoni mwa
zana zilizokamatwa na kuteketezwa ni pamoja na mitumbwi, nyavu,na baruti katika
forodha nane za Mtakuja,Nunka,Uwanja wa
Ndege,Mchangani,Chafundika,Masuche zilizopo wilayani Momba mkoani Mbeya na
wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kufuatia
kufunguliwa kwa Ziwa hilo Libenanga alisema halmashauri imeamua kulifanya Ziwa
hilo kuwa ni chanzo kikuu cha Mapato na kuwa wavuvi wote wanaovua ziwani humo
watapaswa kuwa na leseni ya uvuvi ikiwa ni pamoja na kusajili vyombo vyao vya
uvuvi.
‘’Kila mvuvi
anapaswa kuwa na leseni ya uvuvi itakayotolewa kila mwaka, kwa sh.16,000,chombo
kinasajliwa mara moja kwa sh.16,000,matumizi ya leseni ni ya mwaka mmoja,’’alisema
Libenanga.
Akizungumza
wakati wa kufunguliwa kwa Ziwa hilo Mkuu wa Wilaya ya Momba Saideya alisema
kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kulitunxza Ziwa hilo ambalo limekuwa ni
sehemu ya chanzo cha mapato cha Halmashauri ya wilaya hiyo.
Aliwataka
wananchi kudhibiti mifugo yao ili isiingie
ovyo ziwani na kutunza vyanzo vyake ili kutoathiri uchumi wa wakazi wa maeneo
yanayolizunguzuka hivyo ni vyema kila mwananchi akawa mlinzi wa kuhifadhi uoto
wa asili ambao umeanza kuwa kivutio
pembezoni mwa ziwa hilo.
Post a Comment
Post a Comment