Wanafunzi wa sekondari Forest wakionesha namna ambavyo walikuwa wakiadhibiwa na walimu baada ya kushindwa kutoa rushwa ya sh.500 katika chumba cha Guantanamo
WALIMU
wawili wa shule ya sekondari Forest ya Jijini Mbeya ambao awali walidaiwa
kuwalazimisha wanafunzi wa shule ya hiyo kutoa rushwa ya sh. 500 kwa kuchelewa
shuleni na kupewa adhabu katika Jela iliyopewa jina la Guantanamo wamehukumiwa
kifungo cha miaka mine jela kila mmoja.
Walimu hao
Faustin Robert(36) na Simon Mwasote(41) walidaiwa kutenda kosa hilo Machi 4
mwaka 2013 ambao kwa nyakati tofauti waliwalazimishwa wanafunzi kutoa sh. 500
kila mmoja kwa makosa ya kuchelewa
shuleni.
Hukumu ya kesi
hiyo iliyofikishwa kwa mara ya kwanza
mahakamani hapo Machi 27 mwaka jana imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mkoa Michael Mta ite
mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKUKURU Joseph Mulebi.
Akitoa hukumu
hiyo Hakimu Mtaite alisema kuwa washitakiwa wamekutwa na jumla ya makosa manne
kwa pamoja ambapo mshitakiwa wa kwanza
Robert alikutwa na kosa moja la kupokea rushwa y ash.500 kutoka kwa
mwanafunzi wa kidato cha Nne Samwel Mbilinyi.
Hakimu Mtaite
alisema kuwa mshitakiwa wa pili Mwasote alikutwa na makosa matatu ya kupokea
rushwa ya sh.500 kutoka kwa wanafunzi watatu ambao ni Evelina James aliyekuwa
akisoma kidato cha Nne wakati huo,Faraja Kasian na Recho Mwasiposya waliokuwa
wakisoma kidato cha tatu.
Alisema kuwa washitakiwa
kwa pamoja walitenda kosa ikiwa ni kinyume cha kifungu namba 15 (1)(a) cha
sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007 ambapo watuhumiwa kila mmoja wanahukumiwa
kwenda jela miaka 4 kila mmoja ama kulipa faini ya sh.500,00 kwa kila kosa.
Kulingana na
hukumu hiyo mshitakiwa wa kwanza Robert alihukumiwa kwenda jela miaka minne au
kulipa faini ya sh. 500,000 ambapo mshitakiwa wa pili Mwasote naye alihukumiwa
kifungo cha miaka minne jela kwa makosa yote ama kulipa faini ya sh,milioni
1.5.
Awali Mwendesha
mashtaka wa TAKUKURU Mulebi aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa
washitakiwa kutokana na kukosa maadili ya kazi pamoja na kuonywa na Bodi ya
shule hiyo na kwamba mmoja wa walimu hao alimpiga na kumvunja mgongo mwanafunzi
aliyelazimishwa kuweka kichwa chini miguu juu wakati wa utekelezaji wa hukumu
katika chumba kilichopewa jina la Guantanamo.
Hadi tunakwenda
mitamboni washitakiwa hao walikuwa bado hawajalipa faini na hivyo kuanza
kutumikia kifungo cha miaka minne jela kwa kila mmoja.
|
Post a Comment
Post a Comment