Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas KANDORO akitoa baraka za safari kwa wanahabari ofisini kwake leo asubuhi juu ya ziara yao ya kimafunzo katika nchi za MALAWI na ZAMBIA katikati ya mwezi Agosti |
RC KANDORO akisikiliza kwa makini azma ya safari ya kimafunzo ya wanahabari nchini MALAWI na ZAMBIA |
Baadhi ya wanahabari waliofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa leo saa moja asubuhi |
Mmoja wanahabari Felix MWAKYEMBE akielezea mpango mkakati wa wanahabari juu ya azma yao ya kutembelea nchini Malawi na Zambia katikati ya AGOSTI. |
Mkuu wa Mkoa Abbas KANDORO akifuatilia kwa makini maelezo ya wanahabari juu ya ziara yao katika nchi za MALAWI na ZAMBIA. |
Wanahabari wakipewa Usia na Mkuu wa MKOA juu ya safari yao nchi za MALAWI na ZAMBIA |
''Safari yenu, mna-cross Border zingatieni maadili ya taaluma yenu huko nchini kwa watu, hata hivyo mnapaswa kuwa Borden to Horizontals'' |
Mmoja wa wanahabari Christopher NYENYEMBE akiagana na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa baada ya kumaliza mazungumzo na kuwatakia maandalizi mema ya safari |
Awali kabla ya kuingia ofisini kwa mkuu wa mkoa, wanahabari walifika ofisi ya Msaidizi wa MKUU wa mkoa MASAYA na kuzungumza naye machache juu ya safari yao. |
Katibu wa Mkuu wa mkoa MASAYA akiwasikiliza wanahabari kabla ya kukukatana Mkuu wa Mkoa. |
MKUU wa mkoa
wa Mbeya Abbas Kandoro na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa Asumsio Achacha wamewataka
waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya ambao wanajiandaa na safari ya nchini Malawi na Zambia kuwa wawakilishi
na mabalozi wazuri katika kuutangaza mkoa wa Mbeya na Tanzania kwa ujumla.
Kandoro na
Achacha walizungumza na wanahabari hao kwa nyakati tofauti leo asubuhi
walipotembelewa ofisini kwao kwa nia ya kuelezea azma ya safari yao katika
nchi za Malawi na Zambia katikati ya Mwezi Agosti.
Ziara hiyo
ya wanahabari imeandaliwa na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya
ambao hujihusisha na habari mbalimbali za kijamii ikiwemo masuala ya utafiti juu
ya mahusiano baina ya jamii
ya ndani na nchi jirani.
Akizungumza na
wanahabari hao baada ya kupewa taarifa za safari hiyo Mkuu wa Mkoa Kandoro
alisema kuwa suala la mahusiano baina ya nchi na nchi ni jambo linalopaswa
kuwekewa kipaumbele hususani katika mgogopro unaoripotiwa juu ya Tanzania na
Malawi.
Alisema kwa
kutumia fursa ya ziara ya wanahabari nchini humo itasaidia kuondoa fikra
zilizopo kwamba kuna ugomvi baina ya nchi mbili hizi na kuwa mbali na ziara
hiyo ya kimafunzo wanahabari wanatakiwa kuenda mbali zaidi ili kupata mengi
ambayo yataendelea kuitangaza Tanzania na nchi jirani ya Malawi.
‘’Tumieni
ziara yenu, kujifunza pia angalieni mengine yenye manufaa katika kuitangaza
Tanzania, ‘’Borden to Horizon’’ hii itasaidia hata nchi jirani na Malawi
kujua nini kilichopo Tanzania na kuwavutia,’’alisema.
Pia aliwataka
wanahabari kutumia nafasi hiyo kutangaza fursa na vivutio vilivyopo nchini kwa
nia ya kuwavutia wageni kutoka nchi hizo kutembelea nchini mwetu ikiwa ni
pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo katika kipindi cha mpito kwa
mgogoro unaoelezewa kuwepo kuhusu mpaka wa nchi hizo.
Kwa upande
wake Ofisa Uhamiaji wa Mkoa, Achacha alisema kuwa fursa ya wanahabari
kutembelea nchi jirani za Malawi na Zambia zitaibua upya mahusiano baina ya
nchi hizo na kuwa kwa kutumia kalamu za waandishi wa nchi zote mbili taarifa
zitakazotolewa zitakuwa chanya.
‘’Mengi yanayoripotiwa
ni Hasi, katika ziara yenu na wenyeji wenu wa
huko tutapata taarifa chanya, tumieni fursa hiyo kuelezea hali halisi
ya mahusiano baina ya nchi zetu, nchi yetu haina Vita na Malawi,’’alisema
Achacha.
Awali
akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mwenyekiti wa kamati ya safari ya
wanahabari hao, Ulimboka Mwakilili alisema kuwa azma ya safari hiyo ni ziara ya
kimafunzo iliyolenga kujenga mahusiano baina ya nchi hizo kupitia wanahabari wa
Tanzania na Malawi ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa na vivutio vilivyopo
nchini.
Takribani
wanahabari 25 wanatarajia kuanza safari yao ndefu kuelekea nchini Malawi na kutokea
nchini Zambia na kurejea nchini katikati ya Mwezi Agosti.
Post a Comment
Post a Comment