MKUU wa mkoa
wa Mbeya Abbas kandoro amesifu jitihada
za Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) katika kuboresha makazi na kujenga nyumba bora zinazokidhi viwango na
mahitaji ya wapangaji wake.
Kandoro
alisema hayo wakati akipokea msaada wa mashine 40 za kufyatulia tofali zenye
thamani ya sh. Milioni 18 kwa ajili ya
vikundi vya vijana kutoka halmashauri 10 za mkoa wa Mbeya.
‘’Mnafanya kazi
kubwa kuhakikisha wakazi wanapata nyumba bora,Shirika lenu linafanya vizuri
sana, mnastahili pongezi,’’alisema Kandoro.
Alisema kuwa
awali Shirika hilo lilianza kukatisha tama katika utendaji wake lakini kwa
kipindi cha miaka ya karibuni kimejitahidi kurejesha imani kwa wananchi na
wapangaji wake kwa kuimarisha utendaji na mahusiano na jamii.
Alisema
msaada wa mashine za kufyatulia tofali kwa vikundi vya vijana vimeongeza chachu
ya mahitaji ya nyumba bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa
vijana.
‘’Tunahitaji
kupata nyumba bora kwa gharama nafuu, kwa mashine hizi vijana watamudu kufyatua
tofali imara zitakazojengewa nyumba bora,jambo hili litawakusanya vijana pamoja
na kuacha vitendo viovu,’’alisema Kandoro.
Awali
akikabidhi mashine hizo Meneja (NHC)mkoa wa Mbeya
Antony Komba alisema kuwa mashine hizo ni kati ya mashine nyingi zilizotolewa
na Shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia vijana kutokana na kuwepo kwa makazi
duni ya walio wengi nchini.
Alisema
Shirika limeguswa na hali hiyo na hivyo kuamua kuwawezesha vijana ili waweze kutengeneza matofali ambayo watawauzia
wananchi kwa gharama nafuu ili hatimaye wananchi wengi wamudu kuwa na nyumba
bora kwa gharama nafuu.
Alisema
shirika la Nyumba liliziomba halmashauri kuunda vikundi kwa akila halmashauri
iwe na vikundi vinne vyenye jumla ya watu kumi ambavyo vtachagua
viongozi na kufungua akaunti ya kikundi na baadaye watapatiwa mafunzo.
Komba
alisema mbali na kutoa mafunzo Shirika litatoa mchango wa sh. 500, 000 kwa kila
kikundi ikiwa ni mtaji wa kuanzia shughuli hizo ikiwa ni pamoja na kununua
vitendea kazi kama vile saruji.
Alizitaja
halmashauri hizo kuwa ni Chunya,Mbeya, Kyela, Rungwe, Ileje,
Mbarali,Mbozi,Mbeya mjini,Momba na Busokelo.
|
Post a Comment
Post a Comment