Baadhi ya wachezaji wa timu ya CWT mkoa wa Mbeya |
Aina ya kitambulisho kwa wachezaji ambao ni wawakilishi wa michuano ya Shirikisho la Vyama Vya walimu Kusini mwa nchi za Afrika (SATO) ambayo inaanza Agosti 18 nchini Zambia. |
Ofisa Tawala wa wilaya ya Mbeya Geofrey Annania akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CWT mkoa wa Mbeya Nelusigwe Kajuni na Katibu wa CWT mkoa Kasuku Bilago |
Bendera ya TAIFA ambayo imekabidhiwa kwa wachezaji wa timu ya CWT mkoa wa Mbeya kuiwakilisha Tanzania nchini Zambia. |
Nahodha wa timu ya CWT Macmussy Njegite |
Kikosi cha timu ya Soka CWT wakiwa na viongozi |
KIKOSI cha
timu ya soka ya Chama Cha Walimu (CWT)mkoa wa Mbeya chenye jumla ya wachezaji
14 na viongozi wanne kinawakilisha Watanzania kwenye michezo ya Shirikisho la
Walimu Kusini mwa Afrika(South African Teachers Organization(SATO) yatakayoanza
Agosti 18 mjini Livingstone nchini Zambia.
Kikosi hicho
ambacho kinaongozwa na Rais wa (CWT) Gratian Mukoba kinatarajia kukutana na
nguli wa soka katika nchi za Kusini mwa Afrika ambazo ni pamoja na Malawi,
Zambia,Namibia, Botswana,Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini.
Akizungumza
michuano hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wachezaji hao Jijini Mbeya Katibu
wa CWT mkoa wa Mbeya Kasuku Bilago alisema kuwa mkoa wa Mbeya umepata heshima
kubwa kuwawakilisha Walimu wa Tanzania
katika michuano hiyo ambayo inaanza Agosti 18.
Alisema
michezo hiyo inashirikisha Vyama vya Walimu Kusini Mwa nchi za Afrika ambazo ni
mwanachama wa Shirikisho linalowaunganisha
walimu katika nchi hizo(SATO) ambapo michezo hiyo itachezwa kusini mwa
nchi ya Zambia katika mji wa Livingstone.
Kwa upande
wake Kocha mkuu wa timu hiyo ya walimu
Ibrahim Ahaz Kasegese alisema kuwa wachezaji wako katika maandalizi
mazuri ya ushindi ambapo kwa muda wote
walikuwa katika maandalizi ya ya Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara (SHIMIWI).
Alisema kuwa
anajivunia kuwa na kikosi imara ambacho anaamini kitawajengea heshima walimu na
Watanzania ambapo wachezaji wote wa timu hiyo ambao ni walimu mbalimbali wa
shule za msingi na sekondari wana ari kubwa ya kushinda na kurejea wakiwa kifua
mbele kwa kutwaa kombe.
Akizungumza kwa
niaba ya serikali wakati akikabidhi bendera ya Taifa kwa timu hiyo Ofisa Tawala
wa wilaya ya Mbeya Geofrey Annania alisema kuwa mbali na kushiriki michuano
hiyo na matumaini ya ushindi, washiriki hao wanapaswa kuutangaza mkoa wa Mbeya
na Taifa kwa ujumla.
Alisema
michezo hiyo itaimarisha na kuongeza undugu na ujirani mwema baina ya nchi
washiriki na kuwa fursa hiyo itumike kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma katika
masuala ya elimu na kuongeza chachu ya mafanikio kwa kuambukizwa na nchi
zilizopiga hatua kielimu kati ya nchi hizo.
‘’Tumieni
fursa hii kujifunza na kubadilishana uzoefu kitaaluma ili tuongeze weledi
katika ufundishaji mashuleni,’’alisema Annania.
Kadhalika
alishauri CWT ijiwekee mikakati ya kuunda timu ya kudumu ambayo hatimaye
itapata fursa ya kushiriki michuano ya ligi mbalimbali na baadaye kushiriki
ligi kuu kama zilivyo timu nyingine zinazocheza ligi ya Vodacom.
Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni Josia Kasasi, Bahati Mgaya,Bakari Antony,Narsis
Maseta, Diwadha Mrabyo,Nicholas
Kelion,Bahati Mwakinga na Philipo Owden.
Wengine ni
pamoja na Salum Zacharia,Macmussy Njegite ambaye ndiye Kapteni wa timu hiyo,Mwashilindi
Mwanifumu,Wycleff Komba, Abdul Mpulinga na Yotham Ngailo.
Viongozi
wanaoungana na Rais Mukoba katika msafara wa timu hiyo ni pamoja na Mwenyekiti
wa CWT mkoa wa Mbeya, Nelusigwe Kajuni,Katibu wa CWT mkoa, Bilago,Mwenyekiti wa
CWT Jiji la Mbeya Magdani Sindika na Katibu wake Felix Mnyanyi.
Post a Comment
Post a Comment