Diwani kata ya Halungu wilayani Mbozi mkoani Mbeya Samson Simkoko akielezea muongozo juu ya Mkuu wa wilaya kufanya ubadhirifu fedha za Halmashauri ya Mbozi |
Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro |
Mariam Mtunguja Katibu Tawala mkoa wa Mbeya |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Elick Ambakisye |
Mkuu wa
wilaya ya Mbozi Dkt. Michael Kadeghe ameingia katika kashfa nzito ya ubadhirifu
wa mamilioni ya fedha za Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kudaiwa kulazimisha kulipwa sh. milioni 4 kila baada ya wiki mbili kwa matumizi yake binafsi.
Dkt.
Kaedeghe amedaiwa kudai kulipwa fedha za
halmashauri hiyo mara kadhaa ambapo amekuwa akiandika ‘vi-NOTE’ kwa uongozi wa Halmashauri
hiyo akihitaji kulipwa fedha kwa madai ya safari za kuitwa na Rais Ikulu Jijini
Dar es salaam.
Tuhuma za
DC huyo zimeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo
wakati Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG)alipokuwa akisoma hoja
zipatazo 100 zisizofungwa na Halmashauri hiyo kutokana na kushindwa kwa
utekelezaji wa utendaji wa watendaji wa Halamshauri hiyo.
Kikao
hicho ambacho kilikuwa chini ya Mkuu wa Mkoa Abbas Kandoro aliyeambatana na
Katibu Tawala wa Mkoa Mariamu Mtunguja na wakaguzi wa kutoka (CAG) kiliingia
taharuki baada ya mmoja wa madiwani wa Halmashauri hiyo Samson Simkoko (Kata ya
Halungu) kuomba muongozo wakati Mkaguzi wa serikali Johnson Mbwile akisoma hoja
za halmashauri hiyo.
‘’Mheshimwa
Mwenyekiti naomba Muongozo!! Mkuu wetu wa wilaya amekuwa ni kati ya watu
wanaoirudisha nyuma Halmashauri yetu kwa ubadhirifu wa fedha, ninao ushahidi
mkuu wetu wa wilaya amekuwa akipewa fedha kinyume cha taratibu, anachukua fedha
kwa matumizi ambayo si ya Halmashauri yetu,’’alifafanua.
Kauli ya
Diwani huyo iliungwa mkono na takribani madiwani wote na kuibua taharuki katika
kikao hicho huku Mkuu wa Mkoa Kandoro akiwa ametahayari kwa ujasiri
uliooneshwa na madiwani hao.
Akitoa
ufafanua juu tuhuma hizo alizoibua dhidi ya Mkuu wa wilaya hiyo nje ya ukumbi
wakati akizungumza na waandishi wa habari,, Simkoko alisema kuwa anao ushahidi
juu ya kile alichokibainisha na kuomba iundwe tume kujua ukweli wa jambo hilo
na yeye atatoa ushirikiano kuthibitisha madai yake.
Akifafanua
alisema kuwa ana ushahidi wa nyaraka za mwezi Agosti mwaka huu,
zinazoonesha kuwa Mkuu huyo wa Wilaya amekuwa akipewa fedha za Halmashauri hiyo
kiasi cha shilingi milioni 4 kila mwezi kwa ajili ya kile kilichoelezwa kuwa
amekuwa na safari za kuitwa Ikulu.
“Nipo
tayari kuthibitisha hili, nina ushahidi wa kutosha DC amekuwa akipewa
fedha kiasi cha milioni 4 kila mwezi ukizidisha kwa miezi 12 utapata zaidi ya
shilingi milioni 100, hata hao wanaompa hizo fedha nao wanapaswa
kuwajibika,’’alisema Simkoko.
Hata hivyo
wakati Simkoko akiibua hayo ndani ya ukumbi Diwani wa Kata ya Myovizi Cosmas
Nzowa yeye alidai kuwa kinachozungumzwa juu ya tuhuma hizo ni majungu na kuwa
hana ushahidi wowote juu ya tuhuma alizotoa dhidi ya Mkuu wa wilaya.
Nzowa
alisema kuwa iwapo Mkuu wa wilaya atatuhumiwa kupewa fedha bila utaratibu hata
wao madiwani wanapaswa kuwajibika kwa kuwa nao walinunuliwa pikipiki zenye
thamani ya zaidi ya sh. Milioni 90 bila kufuata utaratibu na kuwa hayo ni
majungu ambayo yanapaswa kupuuzwa.
Akizungumzia
mvutano huo mkuu wa Mkoa wa Mbeya Kandoro, aliwataka madiwani na watendaji wa
serikali kutekeleza majukumu yao kama walivyotumwa kwa maslahi ya umma na
kubainisha kuwa yeye hana tatizo iwapo fedha alizopewa Mkuu wa wilaya
zilitumika kwa ajili ya matumizi ya Halmashauri hiyo hata kama hazikufuata
taratibu.
Aliongeza
kuwa hata hivyo iwapo malipo hayo yalifanyika kwa kificho hatakubaliana
nayo kabisa na kuwa matumizi ya fedha za serikali yana utaratibu wake maalumu
na hayapaswi mtu mmoja kujiamualia anavyotaka.
‘’Kama
malipo haya yalifanyika kwa kificho sitakubaliana nayo,lakini iwapo yalitolewa
kwa kazi zinazohusiana na Halmashauri pamoja na kuwa DC ni mtumishi wa serikali
kuu hili halina tatizo,’’alisema Kandoro.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Elick Ambakisye, alihitimisha kikao hicho
na kumuomba Mkuu wa mkoa kulifuatilia kwa umakini suala hilo kutokana na
hali mbaya iliyopo wilayani humo na kuwa viongozi hao wamekuwa wakiwindana hata
kufikia hatua ya kutishiana kuuwana.
Kwa mujibu
wa taarifa ya CAG, ubadhirifu na wizi wa fedha hizo umetokea katika miradi ya
kilimo, Maji na ujenzi wa maghala na ununuzi wa pikipiki za shilingi milioni 92
bila kuwa na listi wala maelezo.
Post a Comment
Post a Comment